TB JOSHUA IMAGES WI MSG

FLORA MBASHA BIDHAA1

FLORA MBASHA BIDHAA 2

FLORA MBASHA BIDHAA 3

WATCH EMMANUEL TV LIVE

AFRICAN CRYING

AFRICAN CRYING

RUMAFRICA CONTACTS

Monday, July 6, 2015

RAIS JK KIKWETE AWAHIMIZA WAUMINI KUWACHAGUA VIONGOZI AMBAO SIO WAOVU

Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa dini nchini kuwahimiza waumini wao kuwachagua wanasiasa wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu au hata kuukaribia.Amewataka kuepuka makundi ya kisiasa na wasiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu katika kutafuta madaraka kwa thamani yoyote na wawakemee wale wanaotaka kupata madaraka kwa gharama yoyote.

Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 125 tangu kuingia kwa injili katika ukanda wa Pwani ya Tanga na Milima ya Usambara uliofanyika katika Viwanja vya Mbuyukenda jijini hapa.

“Wanasiasa wanaotaka madaraka kwa njia yoyote ile, muwanyanyapae, wakatalieni kwa macho makavu, hawa si watu wema watatufikisha pabaya,” alisema Rais Kikwete.

Alisema hayo baada ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Stephen Munga kumweleza kwamba akiwa mkuu wa nchi anao wajibu wa kuhakikisha Taifa linavuka kwa amani na usalama katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema katika kipindi hiki, viongozi wa madhehebu ya dini wasijiingize katika makundi ya wanasiasa kwa sababu mambo yakiharibika itakuwa hakuna pa kukimbilia.

Aliwataka viongozi wa dini watumie nyumba za ibada kuliombea Taifa livuke salama katika kipindi hiki kigumu badala ya kuwapangia vyama au viongozi wa kuwachagua.

“Tunawategemea kuwahimiza na kuwakumbusha kutumia haki na wajibu wao vizuri, muwahimize na kuwakumbusha kuwa watatakiwa kufanya mambo matatu muhimu; Kwanza, kujiandikisha, pili, kujitokeza kwenda kupiga kura na tatu kuchagua viongozi wazuri, wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu na kuukaribia uovu, watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo na kujali masilahi mapana ya jamii husika na nchi yetu.”

“Viongozi wa dini muwe kama mimi, nina wagombea wa urais 42, kama nitaonyesha kuwa upande wa mgombea yeyote kati yao, basi nitakuwa nimeharibu mchakato mzima wa uchaguzi.

“Tusiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu kuwafarakanisha Watanzania. Tuendelee kukemea matumizi mabaya ya fedha, rushwa, hila, ghiliba na hujuma katika uchaguzi. Tunapaswa kufanya hivyo tena zaidi sasa, wakati wa michakato ya ndani ya vyama vya siasa na baadaye wakati wa uchaguzi,” alisema.

Alisema hiki ni kipindi nyeti na kwamba, viongozi wa dini pamoja na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kufahamu kuwa Tanzania haina kinga ya milele ya amani na utulivu, kama itavurugwa haitakuwa lulu ya Afrika tena kama ilivyo sifa yake.

“Tuwakemee wanasiasa wapenda madaraka kwa gharama yoyote, ambao watataka kutumia fedha kununua ushindi au ubaguzi wa rangi, kabila, dini na kadhalika, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga kisiasa.

Nawaomba msiwasikilize wala kuwaendekeza kwani mchezo wao ni mauti yetu. Wakatalieni kwa macho makavu na kwa kweli muwanyanyapae,” alisema.

Rais Kikwete ambaye wiki hii atakuwa na kibarua cha kuongoza vikao vya kuwachuja wagombea kupitia CCM, alisema hawapaswi kukaa kimya dhidi ya watu wanaokiuka maadili na kuchochea mifarakano katika Taifa.

“Hawa si watu wema, watatufikisha pabaya. Hawaitakii mema nchi yetu. Kamwe tusiruhusu wachezee dini zetu ambazo ni mhimili muhimu sana wa amani yetu,” alisema.

Alisema tofauti na ukabila ambao pamoja na ubaya wake, unaweza kuhusisha eneo dogo, dini zinahusisha nchi nzima.

“Hakuna mtu, dini wala eneo litakalonusurika. Tutapoteza ile sifa yetu ya kihistoria ya kuwa lulu na mfano wa amani katika Afrika. Tusikubali kumchukiza Mungu akatukasirikia na kutuadhibu kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu kulizuia lisitokee.

Kwa kweli mambo yakiharibika, hatuwezi kumlaumu mtu mwingine yeyote, bali sisi wenyewe. Katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu, bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe.”

Aliwaomba viongozi wa dini: “Limeni mraba wenu vizuri nasi tulime wetu. Msiwape nafasi viongozi wa siasa na hata wa dini kutumia majukwaa ya dini kuendeleza masilahi yao ya kisiasa na hasa kupandikiza chuki katika jamii.

Msiwe sehemu ya makundi ya wagombea au vyama vya siasa. Mnatakiwa msiwe na upande, muwe juu ya pande zote. Hapo ndipo mtakapofanya vizuri kazi yenu ya ulezi na kuponya Taifa iwapo kutatokea matatizo.”

Kauli ya askofu
Askofu Munga mbali na kueleza historia ya kuingia kwa injili katika eneo la Pwani ya Tanga na Milima ya Usambara, alisema kanisa hilo litaliombea Taifa livuke salama katika Uchaguzi Mkuu...

“Tunakuahidi kukuombea wewe na nchi ivuke kwa amani na salama. Wewe kama mkuu wa nchi una mzigo mzito wa kuhakikisha unatuvusha vyema.”

Alisema kilele cha maadhimisho ya miaka 125 ya kuingia kwa Injili kitakuwa Julai 12, mwaka huu katika Kanisa la Makao Makuu ya Dayosisi mjini Lushoto na zaidi ya vijana 125 watatembea kuanzia Tanga hadi Lushoto kwa kupita njia ambazo Wamisionari walipitia kwa miguu wakati wakieneza injili.

Alisema katika kipindi cha miaka 125, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imeendesha huduma nyingi za kuisaidia jamii ikiwa ni wajibu wake wa kutobagua kwa itikadi za kidini wala rangi.

R.I.P APOSTLE JOHN KOMANYA...ULIONYESHA BIDII ZAKO KUWALETA WATU KWA YESU

Rumafrica inatoa pole kwa ndugu na jamaa wa Mtumishi wa Mungu marehemu Apostle John Komanya. Tunawapa pole Watanzania na watu wa Marekani ambako mtumishi huyu amewahi kufanya kazi yake ya kumtumikia Mungu. Tulipa pole kanisa la CATHEDRAL OF JOY lililopo Marekani na nchini Tanzania kwa kuondokewa na mwanzilishi wa kanisa hilo duniani. Tunatoa pole kwa bendi yake ya Joy Band ambayo ilikuwa bega kwa bega na mtumishi wa Mungu kwa lengo la kuwavuta watu waje kwa Yesu Kristo.

Apostle John Komanya

Rumafrica imepokea kwa majonzi makubwa sana kwa huyu mtumishi wa Mungu. Tunachokumbuka kutoka kwa mtumishi huyu wa Mungu siku za mwishoni kabla ya kifo chake ni jinsi alivyokuwa anajibidiisha sana kufanya kazi ya Mungu, alikuwa akifika hapa ofisini kwetu kwaajili ya kutengeneza matangazo yake ya matamasha, stickers za mafuta ya upako, mabango, tshirts na vitu vingi sana. Alikuwa ni mtu mwenye kutamani sana kuona kazi ya Mungu inafanyika kwa viwango vikubwa sana, alipenda sana kuona matangazo yake yanakuwa katika viwango vya juu sana. Nakumbuka siki moja tulitengeneza poster yake na yeye hakuweza kupendezewa nayo na kutuambia, naomba ufanye upya kwani huyu naye mtumikia ni mkuu sana, akiona kazi yake iko kwenye kiwango cha chini ataniadhibu, kwahiyo tengeza tangazo upya la kiwango cha juu kwani ni tangazo la Mungu. Kama Rumafrica tulijifunza kitu kutoka kwake na kuona anachosema ni kweli kwani Mungu wetu ni wa viwango vya juu.

Apostle John Komanya alikuwa mtu wa utani
Marehemu John Komanya mabaye alimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kuhubiri alikuwa akifika hapa ofisi kwetu, aliomba sana kusamehewa hataka kama hujamkosea, utasikia anasema, "Kaka naomba unisamehe" huku akicheka. Hakika Rumafrica itazidi kumkumbuka mtumishi huyu wa Mungu. Marehemu alikuwa na ndoto za kufanya matamasha Tanzania nzima na aliiomba ofisi ya Rumafrica kuwa pamoja nayo kwaajili ya kurusha matangazo yake hewani wakati akihubiri, tulipanga kuanza Morogoro tarehe 26/06/2015 na baadae kwenda mikoa mingine kwa kazi ya Bwana.

Apostle John Komanya alikuwa mtu wa utani
Katika watu waliokuwa wanajibidiisha katika kazi ya Bwana, marehemu Apostle John Komanya ni mmojawapo, alikuwa akifika ofisi kwangu hata usiku saa tano kufuatilia kazi zake za matangazo, alikuwa hapendi kuona kazi zake zinacheleweshwa, alikuwa anadiriki hata kutoa pesa zaidi ya ile uliyokubaliana nayo ili kufanikisha kazi ya malengo yake on time.

Kilio chake kingine kilikuwa ni juu ya maalibino, alikuwa anaumia sana kuona walemavu wa ngozi wananyanyaswa na ndio maana aliweza kuandaa mkutano wake wa Morogoro kupata fedha kwaajili ya kuwasaidia maalbino na kupinga unyanyasaji kwa maalbino. Marehemu alikuwa anatamani kuona nchi ya Tanzania inakuwa katika utulivu na amani na pia aliamua kufanya tamasha kubwa kwaajili ya kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu kipindi cha UCHAGUZI MKUU 2015.

Kuna mambo mengi sana aliweza kuyaongea na Rumafrica ikiwa ni pamoja na kutunga nyimbo za kulisifia Taifa letu na kuhamasisha watu kuwa na upendo. Ukisoma katika sticker yake hapo chini utaweza kujifunza kitu kuhusiana na KIFO CHAKE....

Rumafrica sasa inapenda kukuonyesha baadhi ya kazi za mtumishi wa Mungu Marehemu Apostle John Komanya alizofanya kwaajili ya kumtukuza Mungu na kutangaza Injili

KAZI ALIZOZIFANYA HIVI KARIBUNI NA RUMAFRICAFriday, July 3, 2015

JENNIFER MGENDI AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUFIKA KATIKA TAMASHA LAKE

Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Tanzania, Jennifer Mgendi amewashukuru Watanzania kwa  kukushiriki tamasha lake la uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa WEMA AKIBA. Jennifer Mgendi ambaye amejipatia umaarufu sana katika kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji na uigizaji wa filamu za Kikristo Afrika Mashariki amewataka wananchi kuzidi kuuunga mkono waimbaji wa nyimbo za Injili kwa kufika katika matamasha wanayoyaandaa ili watu waweze kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.
Mungu azidi kuwabariki sana na azidi kubariki kazi ya mikono yenu kila kuitwapo leo..Ameni
 
 Cosmas Chidumle kushoto akienda sawa na Jennifer Mgendi (katikati)
 Jennifer Mgendi

 Jennifer Mgendi akimtukuza Mungu mbele za Watanzania waliofika katika tamasha hilo
 Albamu ya Jennifer Mgendi ikiombewa na watumishi wa Mungu akiwemo mgeni Rasmi wa pili kutoka kulia


 Mgeni Rasmi Askofu Mkuu wa TAG Dr. Barnabasi Mtokambali akionyesha DVD ya Jennifer Mgendi baada ya kuzinduliwa. Kulia ni Mch. Swai wa kanisa la DCT TAG ambako tamasha hili lilifanyika


MATANAGAZO YA TAMASHA LA JENNIFER MGENDI YALIYOTENGEZWA NA RUMAFRICA
JUMAPILI HAPAKAMATIKI...MARY MGOGO KUSHUSHA UWEPO WA MUNGU..WATAZANIA MSIKOSE KABISA.
EXCLUSIVE: SILAS MBISE AKIONGEA NA MARY MGOGO JUU YA TAMASHA LA JUMAPILI..TUWASIKILIZE SASA

a

Thursday, July 2, 2015

MATUKIO YA TAMASHA LA FLORA MBASHA UBUNGO PLAZA KIPINDI CHA KUSHIKANA MKONO NA MH. FREMAN MBOWE KWA KUNUUNUA DVD YA "NIPE NGUVU YA KUSHINDA"

Kwa muda mrefu sana Flora Mbasha alikuwa na DREAM ya kufanya tamasha lake la uzinduzi wa DVD zake ambazo amekuwa akiziuza kwa watu wengi sana duniani na pia zimetokea kupendwa na watu wengi,  lakini wakati wa Mungu ulikuwa bado haujafika kwa mwimbaji huyu kufanya tamasha.

Flora Mbasha ni mmoja wa wakongwe wa nyimbo za Injili Tanzania na ni mmoja kati ya waimbaji wanaopendwa sana na huduma yake ya uimbaji. Watu wengi sana wamebadilisha maisha yao na wengine kuingia katika ulimwengu wa uimbaji kutokana na uimbaji wake.
Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe (kushoto) akimuongelea Flora Mbasha mazuria anayofanya kwa kazi ya Mungu.

Siku ya tarehe 14/06/2015 saa 8 mchana ndani ya Ubungo Plaza ilikuwa ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka special kwa dada Flora Mbasha kufanya tamasha lake la uzinduzi wa video yake mpya inayoenda kwa jina la MUNGU WA AJABU. Hakika Mungu aliweza kuwatumia watu aliowaona wanaweza kumuunga mkono katika maandalizi ya tamasha lake nao ni The Fadhaget Sanitarium Clinic, Kidoti, Gombo Tours, Clouds TV, Wanawake LIVE, AG Press, ABE Sound, Coca Cola, Rumafrica na wengine wengi kudhamini tamasha lake. Pia kulikuwa na wageni waalikwa na maalumu ambao waliweza kutoa michango yao kwa moyo wa upendo.

Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji wengi sana kama vile Furaha Isaya, Joyce Ombeni, Lilian Kimola, Glory Mainah, Elizabeth Ngaiza, Christopher Mwahangila, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi waliofika kumtukuza Mungu na kumuunga mkono mwimbaji wao mpendwa Flora Mbasha.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa tamasha hili. Mheshimiwa aliweza kuongea maneno yenye kutia faraja na kujenga imani za watu hasa pale alipokuwa akiongelea maisha ya Flora Mbasha kwa ufupi na hasa mapito aliyokuwa akipitia. Maneno yake hakika yaliweza kumgusa Flora Mbasha na kumpa nguvu ya kusonga mbele. Mh. Freeman Mbowe aliweza kuchangia kiasi cha milioni 11 na ushehe kuidumisha huduma ya mwimbaji huyu.

Flora Mbasha aliweza kuitambulisha bendi yake  mpya ambayo atakuwa akizunguka mayo mikoani kufanya kazi ya Mungu. Rumafrica ndio walioweza kuandaa matangazo yote ya Flora Mbasha ili watu waweze kujua ni kitu gani Flora Mbasha anakwenda kukifanya, na pia kuonyesha matukio ya tamasha hilo baada ya kumalizika. Hivi leo unaona matukio haya kwa njia ya picha zilizopigwa na Rumafrica (+255 715 851 523) ili uweze kuona kazi ya Mungu aliyoifanya Flora Mbasha. Rumafrica itazidi kuwaletea tena matukio mengine ya tamasha hili.Flora Mbasha (kushoto) akiwa na waimbaji wa bendi yake wakimsikiliza Mh. Freeman Mbowe

Flora Mbasha (kushoto)
xxxx
Mh. Freeman Mbowe

Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA akitoa maneno machacha kabla ya kuunza kunadi DVD ya Flora Mbasha

KIPINDI CHA WADAU WA FLORA MBASHA KUNUNUA VIDEO YA NIPE NGUVU YA KUSHINDA YA FLORA MBASHA NA KUWEZA KUSHIKANA MKONO NA MGENI RASMI MH. FREEMAN MBOWE.MC. Sarah Mvungi (kushoto) akimsikiliza mdau wa Flora Mbasha akitamka kiasi cha kuchangia huduma ya Flora.


Mama mzazi wa Flora Mbasha akitamka kiasi cha kumchangia mwane kwa kununua DVD ya Nipe Nguvu ya Kushinda ya Flora Mbasha

Mama Mzazi wa Flora Mbasha akipokea DVD ya mwanae kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe ambayo aliweza kujinunua
Muwakilishi wa The Fadhaget Sanitarium Clinic Bwana Lonely akitamka kiasi cha kumchangia Flora Mbasha. The Fadhaget Sanitarium Clinic chini ya Mkurugenzi Dr. Fadhili Emily waliopo Mbezi Beach Afrikana ndio wadhamini wa Tamasha hili.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Lilian Kimola (kushoto) akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe baada ya kuinunua
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Glory Mainah akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe.
Meneja wa Praise Power Radio Bwana George Mpella akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Celline Theophile akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Mch. Maximillia (kushoto)
Furaha Isaya (kushoto) akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Furaha Isaya na Mh. Freeman Mbowe
Mwimbaji kutoka kikundi cha GWT  Bwana David (kutoto) akipokea DVD kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe

BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KUONA MUENDELEZO WA HAYA MATUKIO YA UUZAJI WA DVD ZA FLORA MBASHA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...