RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHINI YA KAPETI: MCH. ELISHA ATISHIA KUMUUA MDOGO WAKE NA MAREHEMU CHIBALONZE KISA UUZAJI WA NYIMBO ZA MAREHEMU.



Nani mwenye haki ya kuuza nyimbo za Marehemu Anjela Chibalonza?Je Ni Mama yake mzazi? Dada yake? Au aliyekuwa mume wake Pastor Elisha Muliri ambaye kwa sasa ameshaoa..... au Mke mwingine?Ugomvi mkubwa umezuka kati ya Mmoja wa Dada wa Marehemu Angela Chibalonza na Bwana Muliri aliyekuwa mume wa Angela,ambapo kila mmoja anachodai ni haki yake kuuza nyimbo za marehemu.

Hali ni tete kiasi cha Muliri kutisha kuua Shemeji yake kama hata koma kuuza nyimbo za Marehemu ambaye Muliri anadai ni mke wake na Shemeji anadai ni dada yake.Kwa maoni yako nani kati yao mwenye haki zaidi ya mwingine kuuza nyimbo za Marehemu Anjela Chibalonza?Dada anamwambia Muliri kifo kiliwatenganisha na umeoa mke mwingine kwa hiyo Angela siyo mke wako kwa sasa na nyimbo zake sisi familia ya Angela ndio tuna haki kuziuza.Naye Bwana Muliri anasema mimi na Anjela tulioana tukawa mwili mmoja hivyo nina haki..

Chanzo cha taarifa Munishi Faustin.

Comments