RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JOHN LISU AFUNGUKA NA KUMWAGA HISTORIA YAKE NDANI YA CLOUDS 360 LEO ASUBUHI KATIKA KIPINDI KINACHOENDESHWA NA EDSON KAMOGA NA DADA KIJA.


John Lisu ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, na hasa ni mwimbaji ambaye humuimbia Mungu kwa kutumia gitaa lake ambalo limefanyika kama ICON yake duniani. Na amebahatika kumpata mke wake ambaye naye anapiga gitaa la base, kwahiyo chemistry yao iko poa sana. Hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mapacha ya watoto watatu. Siku ya leo alikuwa akifanya mahojiano na watangazaji wa Clouds FM 360, Kija na Edson Kamoga na hivi ndivyo ilivyokuwa.

Swali: Tupe historia yako

Ametoka kijijini Singida ambako leo hii ukiambiwa uende utatamani kurudi kutokana maisha magumu. Mimi nilikuwa nalala na wanyama ndani ya nyumba yetu na baadae Mungu alinitoa huko na sasa niko ambako niko.
http://strictlygospel.files.wordpress.com/2014/02/lisus.jpg
John Lisu (kushoto) na mke wake

Swali: Tupe siri ya mafanikio yako

Siri ya mafanikio yangu ni kujituma na hakuna kitu kingine. Hapa duniani Mungu amempa  kila mtu  kipaji chake na unapaswa kukitambua na kukifanyia kazi. Toka mdogo  wazazi wangu walipogundua kipaji change waliniendeleza na mimi baadae nikajitambua kuwa nina kipaji na ndio maana mpaka leo ninakitumia.

Swali:  Ni amekuvutia mpaka ukawa hivi ulivyo katika kipaji chako cha upigaji gitaa.
Mtu aliyenivutia ni juhudi za baba yangu ambaye alijibidiisha kuchoche kipaji change pale alipogundua nina kitu ndani yangu. Baba yangu hakuwa mwanamuziki alikuwa mchungaji. Marehemu baba yangu alikuwa ananipeleka mikutanoni nap engine kunipandisha katika stuli ili kuwapigia watu gitaa na kuimba.

Swali: Tupe historia fupi ya gitaa lako?
Gitaa langu la kwanza lilikuwa limetengezwa kwa mti, galoni na nyuzi. Na baadaye nikawa mchongaji wa gitaa na baadae nikawa nauza magitaa

Edson Kamoga wa Clouds FM 360

Swali: Video zako za uhai na fungua macho ulipiga live au ulirekodi
Mimi muziki ninaupenda sana kwahiyo ninapenda LIVE na zile nyimbo nimepiga live.

Comments