RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MESS JACOB CHENGULA AUNGANA NA WAZEE WA KANISA LA MITO YA BARAKA

Kama ilivyo ada ya mwimbaji huyu wa nyimbo za injili Mess Jacob Chengula kujichanganya na jamii na kushirikiana nayo katika majukumu mbalimba, safari hii aliungana na wazee wa kanisa la Mito ya Baraka mguu kwa mguu mpaka Kigamboni kwa kazi ya Bwana. Huu ni mfano mzuri sana kuona vijana wanafanya ushirikiano na wazee wetu katika kuzukuma gurudumu la kimaisha. Kumbuka vijana wana nguvu za kimwili na uwezo wao wa kufikiri ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa wazee na nguvu za wazee, kwahiyo wanao uwezo wa kutoa mchango wao wa kimawazo na pia kusaidia wazee hawa katika kazi zinazohitaji wafanye. Ninaamini ukifanya hivyo, Mungu wetu wa mbinguni lazima akukumbuke katika maisha yako na hasa ukiwa unafanya kwa mapenzi mema na sio  kufanya ili usifiwe na kujitwalia utukufu. Unapaswa kufanya kwa kumtukuza Mungu na kutenda yale Mungu anakusihi uyatende maishani mwako.

Kulia ni Mess Jacob Chengula akiwa na wazee wa kanisa la Mito ya Baraka Kigamboni.

Binafsi nimependa sana uhodari na upendo aliouonyesha mwimbaji huyu  wa kupoteza muda wake wa kazi na kujiunga na hawa wazee wa kanisa huko kigamboni kufanya yale ambayo waliyatazamia kuyafanya. Ninakutakia maisha mema mtumishi wa Mungu Mess Jacob Chengula na Mungu azidi kuinua karama yako ya uimbaji wako na pia albamu yako ya MUNGU HABADILIKI ikafanyike baraka kwa walio wengi. Amina

Wako katika Bwana
Rulea Sanga

Comments