RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PASAKA KWANGU NI YA BARAKA - RULEA SANGA


Ni furaha na inapendeza sana kuiona siku nyingine, siku yenye upako wa ajabu. Mungu leo atatukuzwa mpaka basi. Tunajivunia kuwa na Bwana Yesu Kristo katika maisha yetu. Najivuna ninapofanya kazi zangu, ninavyotembea, ninavyolala nalindwa na huyu Bwana Yesu Kristo. Jamani kwa Yesu kuna raha ya ajabu sana. Kama hujabahatika kumuonja huyu Yesu basi jaribu leo utaona utamu wake. Mpokee Bwana Yesu aweze kufungua vifungo ulivyofungwa kwa muda mrefu. Umekuwa na mikosi, balaa, nuksi na vitu kama hivyo kwa muda mrefu, lakini leo ukiamua kuungama dhambi zako na kusema Yesu aingie ndani yako utaona mpenyo wa ajabu sana katika maisha yako.

Rulea Sanga wa RumAfrica

Unajua Bwana Yesu yuko pembeni yako sasa anakuita ila sema humsikii kwasababu sauti za shetani zinakusumbua, hebu sogea pembeni na ongea na huyo Yesu wangu na utaamini maneno yangu. Mimi mwenyewe nilipigiwa kelele sana na shetani lakini ilifika kipindi nikasoge pembeni na kuisikia sauti ya Yesu na nikaitii na sasa ninadunda ndani ya Yesu Kristo. Nimemuona Bwana Yesu Kristo akifanya mabo katika kazi zangu, kuna kipindi unapitia unashangaa Yesu Kristo anakuvusha na kukuweka sehemu salama. Ninachoamini mimi katika maisha yangu tangia niingie katika wingu hili la Yesu Kristo ni kuwa na IMANI (FAITH). Ukiamini kuwa hili ninalopitia linakwisha na ukasimamia mistari fulani katika Biblia, ninakuambia utachomoka tu na shtania atafyata mkia wake. Ishi kwa Imani na kuwa mwaminifu mbele za Mungu.

Halafu nilisahua hili, usiwe mtu wa kufuata miuijiza kanisani ila mfuate Yesu Kristo, wala usiwe mtu wa kufuata nyimbo zinazoimbwa na likianza Neno unasepa au unapiga usingizi, nakuambia hapo devil kwake ni full shangwe. Ukiona unasikia hiyo hali kemea na ikiwezekana mshirikishe rafiki yako aliye fit kiroho akuombee muda huo huo...

Mimi nikuache sasa na nifanye yangu siku hii njema ya pasaka...Poa basi na Mungu akulinde na familia yako. Mbona hamnikaribishe na mimi nile hiyo pilau ya leo....????

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
+255 715 851523

Comments