RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INAWATAKIA IJUMAA KUU NJEMA


Muda huu ni muujiza kwako, sekunde hii ni muujiza kwako. Mungu amekupa tena pumzi, hata kama umelazwa au unateseka kwa lolote lakini bado unadunda duniani, unapaswa kumupongeza sana Mungu wako. Hii ni Ijumaa Kuu ya kuelekea Pasaka unapaswa kukaa chini au kujifungua kona fulani ukitafakari ukuu wa Mungu katika maisha yako na sio ya mwingine. Tenga muda wa kufanya ibada private na kusema utakalo kwa Mungu wako. Mi niko angle fulani nikifanya yangu na Mungu wangu, unaweza kuniona mtaa kimwili lakini rohoni niko sawa nikimimbia Mungu wangu na kumshukuru kwa mengi amefanya katika maisha yangu.

Rulea Sanga wa Rumafrica

Binafsi amenitoa mbali na mpaka nilipo ninasema hakika ni ebeneza. Unajisikiaje katika maombi yako ukaniombea na mimi niwe kama wewe ulivyofanikiwa. Usione wifu rafiki niombee na mimi nijenge, niwe na gari kama lako, nioe, niwe na upako kama wako, niende nchi mbalimbali kama wewe, niwe na hekima kama wewe, nizidi kumpenda Mungu wangu na kufanya yaliyo ya Mungu kama wewe. Acha kunizibia rafiki, anza sasa kuniombea na usiwe kauzibe Mungu hapendi kabisa.

Poa mimi nikutakie mema na ninakuombea sasa kwa kupitia blogu yangu hii. Mungu wangu na akubariki, akuwezeshe, abadilishe maisha yako yawe ya mafanikio, uoe na kuolewa, uponywe, uinuliwe, uwe chachu kwa wenye uhitaji, huduma yako iiunuliwe na ifanye baraka kwa walio wengi. Pokea na yale ambayo sijaorodhesha katika maombi yangu, Mungu azidi kuibariki Tanzania na bunge zima na hasa kuwe na amani katika taifa letu la Tanzania, Mungu awalinde watumishi wa Mungu wazidi kufanya kazi ya Mungu kwa kusikia sauti kutoa kawa Mungu na sio kujitungia maneno yao kwa lengo la kuwavuta watu ili watoe masadaka. Mungu akubariki sana.

Wenu katika Bwana

Comments