RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

YELONIMO MWALO AFANYA MAAJABU KATIKA SEMINA YA KANISA LA OVERCOMERS POWER IRINGA

Mungu ni waajabu sana na anaweza kumtumia mtu yeyote katika kazi yake kwa muda wake, ni wewe kujiachia na kuthubu kuwa pamoja na Mungu. Leo hii Yelonimo Mwalo amemkiri Yesu Kristo na kuamua kufanya kazi ya Bwana kwa kujituma na kujinyima sana ili Mungu ajitwalie utukufu wake.

Yelonimo Mwalo

Yelonimo Mwalo amefanyika baraka kubwa sana mkoani Iringa katika semina ya pasaka inayoendelea katika kanisa la Overcomwers kwa Mchungaji Boaz. Semina hii imeanza siku ya jana ambapo watu walikuwa wengi sana eneo hilo. Watu walishangilia na kufurahi pale mwimbaji Yeronimo Mwaro aliposhika kipaza sauti na kuanza kutoa sauti yake yenye mvuto katika uimbaji, hakika mtumishi huyu anafanya kazi ya Mungu. Ni neema ya ajabu sana unapoona watu wameacha kufikiria mambo yao na kujishtukia wanakupigia makofi na kukushangilia kutokana na kile unachokitoa kinywaji kwako kuwa baraka kwao kwa muda huo. Haya yalitokea pale Yeronimo alipoanza kumwimbia Mungu wetu wa mbinguni watu walifurahi mnooooo sana tena sana.

Yelonimo Mwalo akiwa na mke wake Stella Joel

Kumbuka mwimbaji huyu ametoa albamu yake inayoenda kwa jina la AMENITOA MBALI. Albamu hii inafanya vizuri sana, na imekuwa baraka kwa walio wengi kutoka na yimbo zilizomo zenye kufundisha, kuelimisha na kuadibisha. Nyimbo zake zinamguso wa ajabu na zenye kuleta uwepo wa Mungu usikiapo. Mwimbaji huyu amejaribu pia kuimba nyimbo za lugha yake ya Kihehe ambazo zinapendwa na watu wa makabila yote. Ninatambua ulikuwa hujui hili, mwimbaji huyu ameoa mwimbaji mwenzake Stella Joel na kabla ya hapo hakuwa mwimbaji ila baada ya kumuoa Stella Joel aliambukizwa upako wa uimbaji na sasa Mungu ameubariki na kumuongezea maujanja katika kumuimbia Mungu. Hakika ukithubutu kufanya jambo utafanikiwa na utashagaza walio wengi na hasa wale waliosema hutaweza watawashwa na masikio. Kaa miguuni pa Bwana naye atakuinua tu.

la mwisho nataka kukujuza ya kwamba semina hii imeanza siku ya jana na itamalizika siku ya Jumapili katika kanisa katika kanisa hilo la Overcomers Iringa kwa mchungaji Boaz.

Yelonimo Mwalo alipokuwa katika moja ya studio akirekodi nyimbo zake zilizomo katika albamu yake ya AMENITOA MBALI.
Yelonimo Mwalo na mke wake Stella Joel kabla hawajaoana walipotembelea ofisi ya Rumafrica Sinza Afrikasana Dar es Salaama

Unaweza kuwasilina na mwimbaji huyu ambaye yuko tayari kufanya kazi na wewe mahali popote na kwa muda wowote. +255 769571902 au katika Facebook yake Yelonimo Mwaro

Comments