RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ABAMU YA "NAHITAJI KITU GANI" KANISA LA KIJITONYAMA LUTHERANI LATIKISA WANA DAR ES SALAAM


Oliver Israel akiimba ibadani wakati wa uzinduzi huo.

Waumini ndugu jamaa na marafiki waliofika katika kanisa la Kilutheri usharika wa Kijitonyama jijini Dar es salaam, walipata wasaa mzuri wa kumsifu Mungu pamoja na waimbaji mbalimbali waliofika kumsindikiza Oliver Israel mwimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambaye alikuwa akizindua kanda yake ya kwanza ya sauti.

Israel akienda sambamba na mkewe.

Tendo la uzinduzi lilianza katika ibada ya kwanza na kuendelea ibada ya pili na kuhitimishwa wakati wa tamasha kubwa majira ya mchana ambalo mgeni rasmi mwalikwa alikuwa meya wa manispaa ya Ilala bwana Jerry Slaa ambaye alionyesha kufurahia tukio zima la uzinduzi wa album hiyo inayofahamika kwa jina la 'Nahitaji Kitu Gani?'.

Oliver ambaye alipendeza haswa kwa mavazi aliyokuwa amevaa alishikiana vyema na mumewe bwana Israel Mujumba ambaye pia ni mwimbaji na mpigaji wa kwaya ya Kijitonyama, alikuwa akimwitikia mkewe katika uimbaji huo akishirikiana na waimbaji wengine wa kwaya hiyo.

Chini ni baadhi ya picha za uzinduzi huo.

Mheshimiwa meya wa manispaa ya Ilala Jerry Slaa akizindua CD hiyo.

Oliver akimshambulia shetani.

Ilikuwa safi kabisa.

Kucheza nyumbani mwa Bwana raha.

Hakika alipendeza na kazi ilifanyika.

Comments