RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

LEAH AMOSI AFUNGUKA JUU YA TAMASHA LAKE, AELEZEA MENGI KUHUSU MAISHA YAKE


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Leah Amosi akizungumza na Rumafrica amesema sasa amejipanga kisawasawa katika uzinduzi wa albamu yake ya "NAUCHEKA WAKATI UJAO" tarehe 07.09.2014 itakuwa siku ya Jumapili, Uzinduzi huu utafanyika PTA pale Sabasaba kwa mchungaji Katunzi kuanzia saa 7:00 mchana.
Leah Amos

Katika tamasha hili la kipekee kutakuwa na waimbaji watakaomsindikiza Leah Amos kama vile Bahati Bukuku, Edson Mwasabwite, Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Mungu Kwanzan Team, na wengine wengi watakauwepo. Katika tammasha hakutakuwa na kiingilio kabisa, ni wewe kuja na miguu yako na kufurahia pamoja na Leah Amosi siku hiyo. Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Katiba na Sheria Mh. Angel Kairuki

Katika maohojiano haya utaweza kusikia mengi kuhusiana na huyu dada wa Yesu na hasa maisha yake, kwani ameamua kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji, anasemaje juu ya waimbaji wenzake, mipango yake ya baadae, kiu yake ya kumtumikia Mungu. Nnisikumalizie uhondo, wewe msikilize sasa.

Comments