RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAFOTO: IBADA YA KITUO CHA EFATHA TOWN CENTER SIKU YA JUMAPILI 21.07.2014

Inapendeza sana unapoona watu wanaacha kazi zao na kukimbilia katika mikutano ya Injili au makanisani kwaajili ya kusikiliza Neno la Mungu. Hii imeonekana siku ya jana ambapo Nabii Josephate Mwingira alipoweza kuongea machache kwa waumini wake katika kituo cha Efatha Town Center.

Sauti ya Mungu huwa haipotei hata siku moja kwa yule  mwenye nia ya kuisikiliza sauti hiyo na kutii yale ambayo anasikia katika sauti hiyo. Mungu wetu ana njia nyingi za kuzungumza na watu wake, kwa mfano Mungu anaweza kuwakilisha ujumbe wake kwako kwa njia ya mwanadamu, mnyama, au mimea au kitu chochote.

Siku ya jumapili Mungu aliweza kuleta ujumbe wake kwa kumtumia Nabii na Mtume Josephate Mwingira na ni imani yetu ya kwamba watu waliosikia ujumbe huo waliweza kubarikiwa na kufarijiwa. Kama watu wa Mungu tunapaswa sana kusikiliza hizi jumbe zinazotolewa na watumishi wa Mungu kwa njia mbalimbali kama radio, TV, mikutano, makanisani, mitaani na sehemu mbalimbali.

Heshima na utii ni kitu cha bure sana kwa kila mwamini. Tuwaheshimu hawa watumishi wa Mungu na kutosikia yale wanayoyasema watu kwa kuwasema vibaya watumishi wa Mungu. Tukifanya hivyo basi twaweza kuwakatisha tamaa wale wanaotamani kuokoka.

Mungu wangu awabariki sana.
wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 851523








Comments