RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TIMU YA WAINJILISTI WA SAA YA MAVUNO NA MAKANISA YA KIPENDEKOSTE WATAWASHA MOTO WA INJILI KINONDONI DAR..USIKOSE MWANA WA MUNGU

Kazi ya Bwana mara nyingi inafanywa na wale wanaompenda Mungu, wasio mpenda Mungu hawezi kufanya kazi yake kwani hawampendi. Mungu huwapenda sana wale wanaopenda kushirikiana naye kufanya kazi yake. Furaha ya Mungu ni kuona wewe unaishi kwa kufuata taratibu zake na maisha yako ni ya Upendo.

Timu ya Wainjilisti wa Saa ya Mavuno na Makanisa ya Kipendekoste baada ya kuona hilo sasa wameamua kufanya mkutano mkubwa sana Kinondoni ili wewe na mimi tupate kujua na kufahamu kile Mungu anataka kusema nasi kwa kupitia watumishi wake. Mungu mara nyingi hutnmia njia mbalimbali kuwasiliana nasi, na hasa huwatumia wanadamu kwa kuwapa ujumbe kwa njia nyingi kama vile kuhubiriwa, kuimbiwa, kuchekeshwa, ndoto, kuzungumza na nafsi zetu n.k. Wanadamu hawa huandaliwa na Mungu mwenyewe kwani huwaamini na kuwathamini kutokana na uaminifu wao na juhudi zao katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Wakazi wa Kinondoni na Dar es Salaam nzima, watumishi wa Mungu wamebeba ujumbe kwaajili yako na sio kwaajili ya mwingine. Hudhuria mkutano huu ili Mungu aweza kukukumbusha yale ambayo unatakiwa kufanya ili uweza kupata kile unachokihitaji katika maisha yako. Usiangalie miili yao bali angali kile walichokibeba ndani yao kwaajili yako. Iruhusu nafsi yako kutii hiki ninachokuandikia ili siku hiyo iwe ni ya kihistoria maishani mwako. Tumezoea kuhudhuria mikutano mikubwa sana na pengine hatutoki na kila tulichokusudia, leo hii Mungu anataka uwe mmoja ya watu watakaoshuhudia matendo makuu kwa kupitia watumishi hawa wa Mungu.

Nisikuchoshe sana mwana wa Mungu ili nimekupasha habari Njema

Wako katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 851 523


Comments