RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKAMATWA DAR ES SALAAM LEO ...ANGALIA PICHA HAPA

Jamani dunia inaenda wapi sasa? Mbona majanga mengi sana? Kila kuitwapo leo mambo mabaya wanazidi kuongezeka. Kama Wakristo tunatakiwa sasa kusimama na kuomba juu ya hili tukio la kinyama. Taifa la Tanzania sasa tupige magoti mbele za Mungu na kutubu dhambi zetu na dhambi za wengine. Watu wamekuwa wanyama na kuwa na roho za ukatili wa kufikia kiwango cha kuua wanadamu wenzao.

Tumesikia mengi juu ya mauji yanayonyanyika mitaani mwetu, ya kwamba asilimia kubwa ni kwaajili ya kujipatia fedha na wengine katika imani ya kisheti za kutomwamini Mungu bali kumwamini mwanadamu na kumtumikia. Watu wanauana ili wapate fedha kwa njia hata ushirikina.

Jamani tuone taarifa kuhusiana na mauaji hapo chini:-

Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili


Comments