RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BAADA YA KUAHIRISHWA TAMASHA LA ATOSHA KISSAVA KUTOKA NA MSIBA WA MAREHEMU DEOBORA SAID, SASA TAMASHA LIMERUDI TINA KWA KISHINDO.


Mtumishi wa Mungu Atosha Kissava amerudi tena kwa mara ya pili kufanya kazi ya Mungu. Hii inatokana na tamasha lake kuahirishwa kwasababu ya msiba mkubwa uliotokea katika kanisa ambalo alitakiwa kufanyia  tamasha lake la uzinduzi wa albamu ya U Mwema. Kanisa hilo ni la Maisha ya Ushindi lililopo Mabibo External kwa Askofu John Said. Mnakumbuka ya kwamba Askofu Said John alifiwa na mke wake ambaye alikuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Mch. Debora Said, na kutokana na hilo ikashindikana kufanyika tamasha.

Tunaamini sasa kazi mpya imeanza na siku hiyo itakuwa na siku ya kipekee sana katika kumtukuza Mungu kwa kupitia mtumishi wa Mungu Atosha Kissava atakapokuwa anazindua albamu yake ya U MWEMA. Mungu ameweza kumsaidia mwimbaji huyu kuwakusanya waimbaji wenzake zaidi ya kumi na taono amabao watavamia madhabahu ya Bwana na kumtukuza Mungu kwa uimbaji malidadi kabisa. Tunakuomba usikose mtumishi wa Mungu.

Comments