RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHRISS AHAZI ALIYEPIGA NYIMBO YA "JANA IMEPITA " KATIKA ALBAMU YA MADAM RUTI SASA AMETOA NYIMBO ZAKE KALI KATIKA ALBAMU YAKE YA "WAMESAHAU"

Usione kimia m=kingi ukajua watu wamepote...hakuna kitu kama hicho. Baada ya kukaa kimia kwa muda mrefu, Chriss Ahazi ameweza kumaliza kufanya audio CD yake inayoenda kwa jina la "Wamesahau" Albamu hii yenye nyimbo tisa iliyoibwa kwa lugha ya Kiswahili, kikabila kidogo na Kiingereza unamguso wa pekee sana. Binafsi (Rumafrica) nimesikiliza nyimbo hizo nikabaki mdomo wazi kutoka na yale niliyoyasiki katika nyimbo zilizomo katika abmau hii. Ujumbe, sauti na vyombo vimepangwa kisawasawa, na hii inatia moyo kuona vijana sasa wanachangamkia kufanya kazi ya Mungu.

Chriss Ahazi Audio CD Cover
Sasa niongee na wewe mdau wa nyimbo za Injili. Unaonaje ukanunua hii DVD ukasikiliza na baada ya kusikiliza kwa umakini sana, zima radio yake, tafakari yale uliyoyasikia, fanyia kazi kwa IMANI, baada ya hapo subiria majibu kutoka kwa Mungu. Yatii yote yalioimbwa na Chriss Hazi, bila ya kuamngalia umbo la Chriss, tabia, mwenendo, vituko na mengine mengi bali muuangalie huyu Bwana Yesu ambaye ameweza kuweka maneno yake katika Kinywa cha Chriss Ahaz.

Chriss Ahazi Audio CD Cover

Nadhani utakuwa unajiuliza utapata wapi hizi Audio CD ili usikie na uweza kufuatilia yale Mungu ameweka ndani ya kinywa cha mtumishi wake Chriss Ahaz? Kazi ya mtumishi wa
Mungu inapatikana katika ofisi ya Rumafrica Sinza Sokoni, waweza kuwasiliana na hawa jamaa kwa simu +255 715 851 523
Rumafrica imehusika 100% kutengeneza kava hili lenye mvuto wa pekee.MUNGU AKUBARIKI


Chriss Ahazi Audio CD Cover

Comments