RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ELIZABETH NGAIZA AMSHIRIKISHA ATOSHA KISSAVA KATIKA WIMBO WAKE WA "SEMA NAO BWANA"


Kwako wewe usiyemjua mtumisi wa Mungu Elizabeth Ngaiza, huyu ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Huduma yake ya uimbaji alianza baada ya kukutana na Yesu. Kwa wale waliosoma ushuhuda wake kipindi cha nyuma ni kwamba mwimbaji huyu amepitia mengi sana kabla ya wokovu wake huu.Ukitaka kujua zaidi bonyeza hapa.

Elizabeth Ngaiza akiwa ofisini

Katika wimbo wake huu mpya wa Sema na Bwana, Elizabeth Ngaiza ameamua kumshirikisha mwimbaji mwenzake Atosha Kissava katika video yake. Atosha Kissava amecheza kama mwanamke aliyelaaniwa na ndugu zake. Ndugu msomaji wangu nisikumalizie uhondo ila kwa sasa jua tu kuwa Atosha Kissava amefanya kazi na mtumishi wa Mungu Elizabeth Ngaiza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUjWPw5k5-r_OZGpEKkjmm9Z-oMG6c86vCtQeubbt1rn7Dq-SNJp5f9pnZUX1CmYVzuGIzK0Kp3ZMeoIsLRQuRKizVWMko3QFHXiapCy1Vfe3_CuTciCa5jZ_9Th_Jfc0BHjKzRzVXMnCa/s1600/IMG_2749.JPG
Atosha Kissava ndani ya ofisi za Rumafrica

Akiongea na Rumafrica, Atosha Kissava amesema amejipanga vizuri sana kuleta uhalisia wa nafasi atakayoicheza katika wimbo huu ili watu waweze kuokoka na kumjua huyu Mungu kwa kupitia wimbo wa Elizabeth Ngaiza. Atosha Kissava alimshukuru sana Elizabeth Ngaiza kwa moyo wake wa upendoa na kumuona Atosha Kissava anafaa katika clip atakayocheza. Waimbaji ni wengi sana na waigizaji ni wengi sana Tanzania, lakini Elizabeth kwa neema ya Mungu alimuona Atosha Kissava peke yake anayweza kufaa kucheza sehemu hii ya mwanamke aliyelaaniwa.

Rumafrica iko mbioni kumtafuta waimbaji hawa na kufanya nao mahojiano ili kujua mengi kuhusiana na wimbo huuambao unaonekana utakuwa na ujumbe mzuri sana kwa jamii yetu inayotuzunguka. Kitu nilichojifunza ni kwamba mwimbaji Elizabeth Ngaiza ameonyesha ushirikiano na waimbaji wenzake katika kazi zake na huu ni mfano mzuri sana na hatuna budi kama waimbaji kuufuata.

Unaweza kuwasiliana na Elizabeth Ngaizi kwa Barua Pepe elizabethngaiza@gmail.com

Comments