RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC KUFUNGUA TV NA RADIO. RUMAFRICA KURUSHA VIPINDI VYA GOSPEL KATIKA TV51 NA RADIO 51

Hii ni baraka kwetu Watanzania kwa kupata mkombozi wetu ambaye atalikomboa Taifa la Tanzania katika upande wa kusambaza habari za ukweli kwa Watanzania na watu wote duniani. Mungu ameweza kumpa maono ya ajabu sana Mkurugenzi wa vituo hivi vya utangazaji Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic iliyoko Mbezi Afrikana hapa jijini Dar es Salaam.


Rulea Sanga akiangalia mitambo ya kisasa ya kituo cha TV51 (Transmission) siku ya Alhamisi katika ofisi za The Fadhaget Sanitarium Clinic kwa Dr. Fadhili Emily

Si kazi rahisi kumiliki radio na TV kwa maisha ya sasa kama huna huyu Mungu wetu. Kumbuka Dr. Fadhili Emily ni muumini mzuri sana wa makanisa ya Kisabato. Mbali na uumini pia Mungu amempa neema ya kuwatibu wagonjwa kwa njia ya kutumia mimea na matunda, na watu wengi wamepokea uponyaji.

Logo ya TV51

Tuache hayo... TV hii mabyo kwa sasa iko Online ikiboreshwa na kuwekewa mitambo kikamilifu ili siku ikifika isiwe longolongo. Si muda mrefu TV hii na radio vitakuwa hewani na mtafurahi utamu wa vipindi vingi vikiwemo vya kisanysi zaidi.

Rulea Sanga amebahatika kuwa mmoja wa watangzaji wa kipindi cha Gospel katika TV hii ya kimataifa na pia huduma yake ya Rumafrica itakuwa ikirushwa katika TV hii pendwa. Kuna mambo mengi utaweza kubarikiwa katika kipindi hiki cha kumuia Bwana wetu Yesu Kristo. Tunaamini watu watakwenda kupona na kufunguliwa kwa jina la Yesu Kristo.

Unaweza kuingia Online sasa kwa kubonyeza hapa TV51

Comments