RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASANJA MKANDAMIZAJI NA WAIMBAJI WA GOSPO ZAIDI YA 15 KUVAMIA JUKWAA MOJA KATIKA DVD LAUNCH YA ATOSHA KISSAVA JUMAPILI HII.

Kama unavyomuelewa Masanja Mknadamizaji, mara nyingi huwa hakosei kabisa anapokuwa amekabidhiwa mic na kuachea makombola yake ya maneno ya kuvunja mbavu zako kwa kicheko. Msanii huyu wa Ze Komedi Orijino amekuwa kivutio kikubwa sana kwa Watanzania kwa kuchekesha kwake, mbali na kuchekesha pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili, na kutoka na hilo Jumapili hii ataachia masongi yake ambayo yana ujumbe wa Mungu na fuluuu vituko ukisikiliza na ukibahatika kuona DVD zake. Mungu hakuachia hapo kumtafutia kipaji kingine, Masanja Mkandamizaji pia ni Mchungaji Mtarajiwa ambaye hutembea mitaani kutangaza injili, tunatumaini Jumapili hii ataweza kutoa Neno la Mungu ili mimi na wewe IMANI yetu izidi kukuwa
Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji)
Kwahiyo sioni sababu ya wewe kukosa raha hizi za dunia kwa kufika na ndugu yako au rafiki yako kumuunga mkono Atosha Kissava ambaye Mungu ameweza kumsaidia kufanikisha kurekodi albamu yake mpaya ya UMWEMA. Kutakuwa na waimbaji wengi sana kama unavyowaona katika tangazo hilo hapo chini lililotengezwa na RUMAFRICA FOR ALL NATIONS (+255 715 851 523)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwFUOVV9l7kZmTeNHIuNf2KJE9hJGlUJCKBK_vNmE8Urp_PdlS0Hg8sgPKiWQWraJha2TA5YvN3ZG_W9y4C_trFVE8UsXFyOsUSF4fCrh2Oe5F69wjo1zmrhILy5L0gjDzXe5D1Dp6CB6Y/s1600/Atosha-Kissava---DVD-Launch-Poster2.jpg

Comments