RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI EVAREST T. SHABAN WA KANISA LA JESUS DELIVERANCE CENTRE AMEKUANDALIWA SIKU 7 ZA UKOMBOZI NA UPONYAJI -TEGETA PWANI DAR ES SALAAM

Baada ya watu kuonewa na huyu shetani kwa muda mrefu sana, sasa Mungu kwa kupitia mtumishi wake Mchungaji Evarest Shaban atawasha moto wa Injili akishirikiana na watumishi wa Mungu kutoka mataifa mbalimbali kama vile Uganda, Tanzania na Kenya. Waimbaji mbalimbali watachukua nafasi zao za uimbaji kwaajili ya kumtukuza Mungu na kumzomea adui mkubwa duniani aitwaye shetani mwenye jina baya kuliko yote duniani na mbinguni. Siku hiyo itakuwa ni siku ya pekee sana, watu watabarikiwa na kuinuliwa, watu wataokoka siku hiyo.


Mkutano utafanyika katika kanisa la Jeus Deliverance Centre Tegeta Pwani. Panda magari ya Boko/Bunju shuka njia panda ya Chanika uliza ofisi za serikali za mitaa utaonyeshwa kanisa. Kazi ya Bwana itaanza siku ya tarehe 01 hadi 07/09/2014 kuanzia saa 9:30 jioni -12:00 jioni. Mawasiliano yetu ni + 255 716 968 033 au +255 765 034 353

Comments