RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MFAHAMU MESS JACOB CHENGULA KIUNDANI KWA KUPITIA MAHOJIANO HAYA YALIYOFANYWA NA RUMAFRICA ONLINE TV...

Kwako wewe usiyemfahamu Mess Jacob Chengula (mwimbaji wa nyimbo za Injili), leo hii Rumafrica Online TV ilimsaka mwimbaji huyu na kukaa naye chamber kwa maongezi zaidi. Katika dodossa dodosa na kumbana sana ili kujua undani wa maisha yake, Mess Jacob aliamua kuachia uzi na kufunguka na kuweka wazi historia ya maisha yake toka alikotoka Makete kwao mpaka hapa Dar es Salaam.
Huwezi amini ya kwamba mwimbaji huyu alishawahi kuwa promota mkubwa sana wa nyimbo za Bongo Fleva, ameshika pesa nyingi sana akiwa mdogo, ameoa mwanamke akiwa mdogo sana, hajasoma elimu ya sekondari na hata ya msingi hajamaliza, ni mwimbaji mwenye mafanikio makubwa sana, amemiliki magari akiwa mdogo sana, ameshaenda hata kwa waganga enzi zake kabla ya kumpokea huyu Bwana Yesu Kristo, alishafilisika mpaka marafiki zake na ndugu zake wakaanza kumkimbia.

Nabii Flora Peter akimbandika pesa katika uso wa Mess Jacob Chengula baada ya kuimba vizuri sana

Baada ya kukutana na Yesu milnago ya mafanikio ndipo ilipoanza kufunguka na sasa ni mwimbaji ambaye ana mafanikio makubwa sana na anazidi kufanya vizuri katika kazi ya Bwana.

Mess Chengula (kushoto) akiwa na Masanja Mkandamizaji

Sasa ni muda wako wa kumsikiliza na utajua mengi na kujifunza mengi, KARIBU

Comments