RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MMAREKANI, ALINE VYUKA ANATEGEMEA KUACHIA ALBAMU YAKE YA "NI SALAMA" ILIYOFANYIWA TANZANIA

Aline Vyuka ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Marekani, ila Tanzania ameizoa sana kwani alishawahi kuishi sana hapa Bongo. Mungu ameweza kumpa kibali cha kumtumikia kwa njia ya uimbaji. Mbali na kuwa na majuku mengi ya hapa duniani lakini ameamua kutii ile neema ya Mungu aliyopewa kwa kusudi lake Mungu. Hii ni changamoto kwetu sisi ambao tumepewa neema ya uimbaji lakini hatuifanyi kazi, na kama tunaifanyia kazi basi kwa kiwango cha chini sana mpaka watu wa upande mwingine wa Kristo wanatucheka. Tukumbu ipo siku tutajibu mbele za Mungu kutokana na uvivu wa kufanya kazi ya Mungu kwa bidii na uaminifu.

Aline Vyuka DVD Cover mbele

Turudi kwa dada yetu Aline Vyuka ambaye ameweza kufanya shooting ya video yake hapa nchini Tanzania akiwa na mwenyeji wake Emmanuel Mabisa. Kazi yake ni nzuri kabisa kwani ametumia mazingira ya Kitanzania zaidi. Aline Vyuka ana uraia wa Marekani kwa muda mrefu sasa, kwahiyo kama wadu wa kazi za Mungu tuna kila budi ya kumuobea dada yetu azidi kufanya kazi ya Mungu kwa namna ya pekee ili watu waweze kuokoka na kumfuata huyu Bwana wetu Yesu Kristo. Tuache kuoneana vijembe tunapoona mwenzetu anafanikiwa kwani tukifanya hivyo tunamchukiza Mungu na ni dhambi mbaya sana.
Aline Vyuka DVD Cover nyuma


Kama ungehitaji kuwasiliana naye kwa kazi ya Mungu, basi piga simu hii Marekani 6052018124  Tanzania +255 717 025 328. Facebook: Aline Vyuka, Barua pepe: alinedukunde@hotmail.com. Cover limetengezwa na RUMAFRICA: +255 715 851523


Aline Vyuka DVD Cover

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 851 523

Comments