RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII YASPI BENDERA ATINGA GLOBAL, ATOA UTABIRI KUHUSU UGONJWA WA EBOLA


NABII wa Kanisa la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo eneo la Yombo Buza-Kipera jijini Dar, Yaspi Paul Bendera, ametembelea ofisi za Global Publishers LTD zilizopo Mwenge, Bamaga, Dar hivi punde na kutoa utabiri kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Ebola hapa nchini.

Nabii Yaspi Paul Bendera akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya mahojiano.

Katika utabiri wake, Nabii Yaspi amesema watu 50 watapoteza maisha kwa ugonjwa huo, wakiwemo madaktari wawili na mbunge mmoja. Nabii huyo amesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo bado haujaingia nchini lakini unaweza kuingia muda wowote kuanzia sasa iwapo watu wataendelea kutomtii Mwenyeji Mungu.



Nabii Yaspi akijibu maswali ya wanahabari wa GPL (hawapo pichani), mbele ya kamera za Global TV Online.


Nabii Yaspi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GPL kutoka kulia ni Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (IT), Clarence Mulisa na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amran Kaima.



Nabii Yaspi akiwa katika picha na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.


Nabii Yaspi akipozi na Mwandishi Nyemo Chilongani wa GPL.

Comments