RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIKILIZA ALICHOKISEMA MAREHEMU ORIDA NJOLE AKIONGEA NA RUMAFRICA ONLINE TV ENZI ZA UHAI WAKE

Sina maneno mengi ya kusema juu ya marehemu Orida Njole. Alikuwa mtu wa karibu sana na ofisi yetu ya Rumafrica, alipenda sana ushirikiano katika kazi ya Bwana, alipenda sana kuweka habari zake katika mitandao ikiwa ni njia mojawapo aliyokuwa akifikiri itasaidia sana kusambaza ujumbe wa Mungu duniani kwa haraka na kwa gharama nafuu sana. Tunamuomba Mungu wetu azidi kuwa naye huyu ndugu yetu na rafiki yetu Orida Njole
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsDGhjhTNmVzQ2mmC_a6p1W2j4tb1E_JHHDWMnGifQ8-oM1AgJa5T94F1onUr2Xq5oAyZSYT3KXR5hGeavqXk5j3jaqezMQL868cnZY_-1b3apcEn1AGZf7vlLftOtteI4QaASt6eQ1h0Z/s640/Orida3.jpg
Marehemu Orida Njole alivyokuwa ndani ya ofisi ya Rumafrica miaka miwili iliyopita, akiandaa coner la Audio CD ya Duniani Tuwapitaji

Leo hii Rumafrica imeona ni vizuri ikakuletea maneno machache aliyoweza kuyaongea marehemu Orida Njole enzi ya uhai wake juu ya wanamuziki wa nyimbo za Injili na ujio wa albmau yake ya "Duniani Tuwapitaji" Sikiliza sasa


AUDIO CD COVER LILILOTENGENEZWA RUMAFRICA LA MAREHEMU ORIDA NJOLE
Rumafrica inazidi kuwapa pole ndugu na jamaa wa marehemu Orida Njole na tunaamini ipo siku tutamuona akimlaki Mungu mawingu. Tuzidi kufanya mema ili siku ya mwisho tukakutanae naye huko mbinguni kwa Baba. Tuwe na upendo na tusigombane bali tusaidiane na kufanya yale Mungu ametuagiza katika kitabu chake kitakatifu. Tuwasikilize watumishi wa Mungu yale wanayotuambia kwa kupitia nyimbo zao, mahubiri yao, na njia mbalimbali wanazotumia kuleta ujumbe wa Mungu kwetu, na tusiishie kwuwasikiliza tu bali tufanyie kazi. Mungu awabariki sana wana wa Mungu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_svQsJpseJC6DBztLdm49QrRk_0TpwVUfEcefs4M8SNNpfntIBDhqu1oBJbgfQZcynO1ncz6N8yoj_xpUaFiioeNV4dWHXtFOAgVL8Ba5mZ6fn_aEu_PwdTK9ubNHjm258y4F7VJblpIz/s640/Orida-Njole-CD-Cover-Paper+A.jpg

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSdi83SejNvh41KdrDcCg9Dr4DeLsNPl8qhC1NvQeYz3CEBSAQF0w3amXbv7BE8jvwnRuI973CAKwcQfPaM6wxPAVHIwjjBCQoQyRLBUHs7TVXo9OHvO6gYue8rSPMgeCY7PT_NZPnGO9a/s640/Orida-Njole-CD-Cover-Paper+B.jpg

Comments