RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAARIFA KWA MABLOGA: TUACHE TABIA YA UCHOYO KATIKA HABARI, TUACHE KUHARIBU PICHA KWA KUWEKA MAJINA MAKBWA YA BLOGU ZENU.

Inasikitisha sana kuona bloga amabaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha habari inafika mbali kwa kutumia njia mbalimbali. Leo hii baadhi ya mabloga wanazuia watu wasiweze kukopi habari zao katika blogu zao wakati wao wanakopi habari kutoka kwa mabloga wengine. Hii ni tabia mbaya na sio maadili mazuri kwa waandishi wa habari.

Mabloga tupo kwaajili ya kusambaza habari zifike mbali na sio zibaki tu katika blogu yako tu. Acha tabia ya kubania habari wakati na wewe unakopi kutoka kwa wenzako. Jamii yetu inatushangaa sana kuona tumekuwa bahili hata katika habari, Je, kingekuwa chakula si watu wangekufa njaaa!!!. Haipendezi kabisa na ni aibu sana. Utakuta tu habari nyingi amekopi kutoka kwa blogu fulani na kupesti katika blogu yake, halafu yeye mwenyewe kazuia wengine wasikopi. Hebu ona aibu rafiki yangu.

Sio kila mtu anaweza kupata habari zote duniani, kwahiyo wewe unavyopata habari fulani na ikaonekana itasaidia jamii basi na sisi tunakusaidia wewe kuisambaza ile habari iwafikie watu wengine wapate kujua ni kitu gani kinaendelea duniani.

Pia kuna mabloga wengine ambao wamekuwa wakizichafua picha wanazozipiga kwa kuandika majina ya blogu zao ili waonekane wao ndio walizozipiga zile picha. Hii pia sio tabia nzuri wani unavyofanya hivyo unachafua picha na picha inakosa ule mvuto wake. Mbali na hilo pia kuna watu wanatamani kuitumia ile picha katika matangazo mbalimbali, sasa ukiweka jina la blogu yako ile picha inakuwa hafai kabisa. Tuache hizo jamani tusiwe wabahiri kiasi hicho jamani. Itafika kipindi hata tangazo la tamasha utatamani kuweka jina la blogu yako. Kama ungependa kuweka jina lako ili uonekane wewe ndiye uliyepiga ile picha basia andika maandishi madogo chini yake kama wanavyofanya GLOBAL PUBLISHER ili picha ibaki na mvuto.

Hii tabia imeingia hata katika blogu za wakristo nao wamekuwa na tabia mbaya ya kuweka majina ya blogu zao katika picha, maandishi makubwaaaaa mpaka yanaharibu utamu wa picha. Tuache hizo wana wa Mungu sisi tumeokoka tusibaniane, bali tuoneyeshe mfano wa watu wa duniani jamani. Punguza font za maadishi yako ili hiyo picha iweze kutumika katika kazi zingine.

Tuone mfano huu mzuri kutoka kwa Global Publisher ambaye huandika jina la kampuni yake lakini kwa maandishi madogo yenye font nzuri na inavutia kuangalia. Picha hii unaweza kutumia hata katika kazi zingine inapohitajika
http://api.ning.com/files/w3eiFFRDzzdL-QVAVdUaIbfgIDYPuAf5YWhGxCDlTSQNGrxqi8vcQNWPsqeAkS02FOHyzoAfxJt7ALPQi1wEMxGfjOge1Ay1/MTITU42.JPG

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

Comments