RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DVD YA "NAUCHEKA WAKATI UJAO" YA LEAH AMOSI KUZINDULIWA NDANI YA KANISA LA PTA JUMAPILI HII

Kazi ya Mungu itafanywa na watu wenye bidii ya kufanya kazi ya Mungu, Kazi ya Mungu itapendwa na wale wanaompenda Mungu, kazi ya Mungu itasonga mbele na wale wenye mapenzi mema na Mungu. Leah Amosi ni mmojawapo wa hao wanaopenda kazi ya Mungu isiaibike kamwe, wanaotumia mali zao na muda wao kwa kazi ya Mungu, wanao hakikisha kazi ya Mungu inafika mbali, wanaohakikisha Injili inatangazwa kwa njia ya uimbaji.

Mungu ameweka kitu cha pekee kwa mwimbaji huyu kutoka Tanzania, huduma aliyonayo ni ya aina yake, uimbaji alionao ni wa kipekee kabisa, sauti yake na mpangilio wa maneno katika nyimbo zake ni wa kipekee kabisa. Hakika Mungu atabaki kuitwa Mungu. Na Mungu anamtumia kama chombo chake kuleta ujumbe kwetu sisi wanadamu

Jumapili ya hii itakuwa ni siku yako ya kipekee kushuhudia matendo makuu ya Mungu kwa njia ya uimbaji kutoka kwa mwanadada wa Yesu aliyeamua maisha yake kuwa kwa Yesu na uimbaji wake ni wa kumtukuza Mungu. Dada huyu aliyoona hakuna faida ya kuimba nyimbo za kijamii bali ni kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu. Kuna vitu ataenda kuachilia katika madhabahu ya kanisa la Askofu Katunzi wa PTA pale Sabasaba na watu wataenda kufunguliwa kwa njia ya uimbaji. Siku hiyo utajua maana ya NAUCHEKA KWAKATI UJAO  una maanisha nini?

Watu wa Mungu, kama siku hiyo utakuwa hauna la kukuzuia kufika mahali pale basi nakuomba sana ufike ili Mungu afanye jambo katika maisha yako kwa kupitia uimbaji wa Leah Amosi. Tumeombewa sana na wachungaji, maaskofu, wainjilisti, walimu, mashemasi, mapadre, sasa ni zamu ya waimbaji kufanya kazi ya Bwana kwa njia ya uimbaji ili wewe na mimi tuinuliwe

Mimi nisikuchoshe sana ila nikukumbushe kuwa kutakuwa na waimbaji wengi sana kama unavyowaona katika tangazo hapo chini




SIKULIZA MAHOJIANO YALIYOFANYIKA NA RUMAFRICA JUU YA MAISHA YAKE NA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE


Wenu katika Bwana
Rulea Sana
wa
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

Comments