RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: LEAH AMOS AMEACHIA NYIMBO ZAKE YOUTUBE SIKU YA JUMAPILI


Mtanzania Leah Amos ambaye anafanya kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu kwa njia ya uimbaji, siku ya Jumapili 27.09.2014 aliweza kuweka nyimbo zake Youtube ili mimi na wewe tuweze kusikiliza ule ujumbe Mungu alimuachia kwaajili ya kumtukuza na pia kujenga na kuinua imani yako ya Kiroho.

Leah Amos akiwa katika ofisi ya Rumafrica Sinza Afrikasana sokoni

Utakaposikia nyimbo hizi na kuchukua ule ujumbe aliouimba na kuufanyia kazi, nina imani utabadilika kiimani na pia hofu ya Mungu itakuwa nawe. Mungu wetu ana njia nyingi sana za kufikisha ujumbe wake kwa watu wake, kwahiyo wewe unachotakiwa na kuuchukua huo ujumbe na kuufanyia kazi kwa vitendo.

Zoezi la kuziweka nyimbo hizo katika youtube limefanywa na watumishi wa Mungu kutoka Rumafrica (+255 715 851 523). Na kama ungependa kufanya kazi ya Mungu na Leah Amosi basi wasiliana naye kwa simu +255 714 494 974. MUNGU WETU NA AKUBARIKI SANA





Comments