RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: MSIKILIZE MWIMBAJI WA GOSPO GLORYMAINA MKONYI ALIYEFUATA IMAN YA MAMA YAKE NA KUGUNDUA KUWA ANAKIPAJI CHA UIMBAJI




Baada ya kuishi na mama yake na kufuata imani ya mama yake, Glorymaina Mkonyi ndipo alipoweza kutambua kuwa Mungu ameweka karama ya uimbaji ndani yake. Glorymaina Mkonyi akiongea na Rumafrica For All Nations alisema, katika familia yake hakuna mtu aliyezawadia karama ya uimbaji ila peke yake hata kama baba ni wa imani nyingie na sio ya Kikristo.

Glorymaina Mkonyi ndani ya Rumafrica Online TV
Hakika ukisikiliza nyimbo za huyu dada utamaamini kuwa Mungu ana watu wake wa kumtumikia hapa duniani. Mungu amesaidia kutoa albamu yake iliyokuwa inaitwa ZAWADI na hivi sasa amebadoilisha jina inaitwa NINARINGA akiwa ana maanisha yeye ana ringa kwasababu anaye Yesu anayemuwezesha kwa kila jambo. Nyimbo hii imekuwa na baraka nyingi kwa watu wengi walioweza kusikiliza na imeleta matuda hasa kwa wale waliouchukua ujumbe huo na kuufanyia kazi.

Glorymaina Mkonyi

Hivi sasa yuko katika maandalizi ya kutengeneza Video yake ambayo alisema atahakikisha video yake itakuwa katika viwango vya kimataifa na sio kiwango cha chini kwani Yesu Kristo ni wa kimataifa na lazima watu wake wafanye vitu vikubwa kama Yeye alivyomkubwa. Hata kama nitachukua muda mrefu lazima nifanye kitu kizuri, alisema Glorymaina Mkonyi.

Glorymaina Mkonyi mbali na uimbaji pia yeye ni mfanyabiashara na ni mama wa mtoto mmoja na mume mmoja. Yupo tayari kufanya kazi ya Mungu na wewe, kwahiyo unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 719 529 444

Sasa ungana nami kusikia historia ya maisha yake ya kimuziki na maisha yake kwa ujumla. Ninaamini ukichukua haya aliyoyasema na kuimba kupitia clip hiyo hapo chini na ukafanyia kazi utabarikiwa. Twende sasa....

Glorymaina Mkonyi na Rulea Sanga wa Rumafrica For All Nations

Comments