RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIGIZAJI WA FILAMU , BLOGGER NA MTANGAZAJI WA CLOUDS TV KIPINDI CHA CHOMOZA JAMES TEMU SASA AMEOA..UKAPELA BYEEE.

Ilikuwa miaka, ikawa miezi, zikaja wiki, zikaja siku, yakaja masaa na hatimaye dakika ya 60 kugonga, ndipo James Temu na bibiye Sia Kimaro waliamua kuaga ubachele na kutimiza ili amri ya Mungu ya kuoa na kuolewa. Hii ni heshima mbele za Mungu na mbele za wanadamu kuona watumishi wa Mungu wanafikia hatua ya kutimiza amri ya Mungu.

Unaweza kujiuliza hawa wanandoa siku ya kwanza wamekutana na kuanza uchumba ilikuwaje na mpaka wakavumiliana na hatimaye kila mmoja kuonyesha uaminifu na upendo katika safari yao ya uchumba. Vijana wengi tunachumbia lakini suala zima la kuoa ni mtihani, na hii ni kutokana na kutoaminiana na kutojiamini, na kingine ni tamaa tu na kutovumiliana. James Temu aliweza kushinda hivyo vyote na sasa ameonyesha mfano kwa vijana tuliobaki.

Harusi hii ilifanyika katika kanisa la KKKT Kijitonyama na baadae tafrija ilifanyika katika ukumbi wa Lulu uliopo Sinza Mapambano Dar es Salaam.

Rumafrica inawatakia maisha mema yaenye furaha na amani.

Picha na Samasasali

Kula mama na ishakuwa hivyo..tufurahie maisha

Heee huyu mpiga picha vipi...mbona ghafla hata sijajiandaa kwa poziii

Hivi kweli imekuwa...Mungu ni mwema

Angalia wanavyocheza na kuselebuka kwaajili yetu

Ngoja nile pozii sasa...

Kula mama hii ni siku yetu haijirudii

Vipi matroni tuenda sawa....basi poa..jina la Bwana libarikiwe..

Comments