RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAMUITA NA MBUNGE WA SINGIDA MH. MARTHA MLATA KUFANYA UMISHENI MKOANI SINGIDA

Wakazi wa mkoa wa Singida sasa ni wakati wenu wa kupokea baraka za Mungu. Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kikiongozana na Mbunge wa Mkoa wa Singida Mh. Martha Mlata watafanya umisheni kwa muda wa siku tatu katika wilaya ya Iramba.  Mbali na umisheni pia kutakuwa na uimbaji kutoka kwa waimbaji siku hiyo watakaomtukuza Mungu. Katika zoezi hili kutakuwa na muda wa kuongea na kuwafariji watu wenye uhitaji na yatafanyika maombi kwaajili yao. Siku ya Jumapili ya wiki hilo kutakuwa na tamasha kubwa sana kwaajili ya kuliombea Taifa la Tanzania Amani na mshikamano. Tunawaomba sana wakazi wa Sindida kutokosa.


Comments