RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA ASHANGAZWA KUONA CLASS MATE WAKE DAVID ROBERT USO KWA USO NA MZEE WA STRAIGHT OF AFRICA (SHAKA SSALI)

Kweli dunia, mlima haikutani ila wanadamu wanakutana. Sidhani kama Davi Robert alikuwa na ndoto ya kuwa siku moja atakuja kukutana na mtu maarufu sana duniani na kukaa naye pamoja huku wakipata kinywaji. Sasa nimeamini kwamba ukifanya kazi kwa bidii na kwa malengo hakika utaweza kuwa mtu mkubwa na maarufu dunia, na utaweza kukaa na wakubwa ambao hukutarajia kuwa ipo siku utakuwa nao. Kazi ikienda na kumcha Mungu itakuweka mahali ambao hukutegemea kuwepoa na utawashangaza walio wengi.

David Robert (kushoto) na Shaka Ssali wa VOA

Nikimkumbuka David Robert kipindi ninasoma naye Jitegemee High School Mgulani tukitaniana, lakini leo hii amekuwa kama siye yule ninayemfahamu, na niliyemfahamu kipindi hicho cha nyuma. Mungu azidi kulinda na kumkarisha na wakuu wote duniani kutoka na bidii yake ya kazi na vile anavyomtumikia Mungu wake anayemwamini.

Leo hii ameweza kukutana na mtu maarufu sana dunia Shaka Ssali ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Voice of America (VOA) kipindi cha Straight Of Africa na kuweza kukaa naye chemba wakijadiliana.

Jamanii nimebaki mdogo wazi ila nasema MUNGU WEWE WAWEZA.