RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

STELLA JOEL KUTIKISA AFRIKA KATIKA UZINDUZI WA DVD YAKE YA HAKUNA MWANAMKE MBAYA


Stella Joel anayetegemea kufanya mambo makubwa ndani ya kanisa la KKKT Ubungo External.  Siku hiyo kutakuwa  tamasha kubwa sana ambalo halijawahi kutokea Afrika likiongozana na maombezi makali sana ya kuvunja kibuli cha shetani na kutokomeza kazi zake zote. Pia kutakuwa na muda wa kuiombea nchi ya Tanzania amani na bara zima la Afrika. Kupitia maombezi haya mimi na wewe tutakwenda kupona.

Tamasha hili kubwa litakuwa na waimbaji wengi sana watakaomtukuza Mungu wetu wa mbinguni kwa sifa. Kumbuka siku hiyo hakutakuwa na kiingilio chochote, ni wewe kuja na kufaidi uwepo wa Mungu. Mbali na kupata baraka za Mungu kwa njia ya uimbaji pi utapata muda wa kuongea na waimbaji na kubadilisha na mawazo na kujua mengi kutoka kwao, utapata muda wa kupiga nao picha kwaajili ya kumbukumbu yako.

Tanzania inaenda kupona kwa kupitia tamasha hili la namna yake. Tunamshukuru sana Mungu kwa kumpa kibali mgeni rasmi Mh. Dk. Dalali Kafume kushiriki katika uzinduzi huu na ibada maalumu ya kuliombea Taifa amani. Katika tamasha hili utamsikia Mbunge wa Singida Mh. Martha Malata ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania akisema jambo juu yako ili utakapoenda nalo nyumbani likafanyike baraka katika maisha yako, pia utasikia akimuimbia Mungu siku hiyo. Nachotaka kusema ni kwamba siku hiyo kutakuwa na mambo mengi sana. Mungu akupe uhai tukutane siku hiyo. BARIKIWA SANA.

Comments