RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

STELLA JOEL KUZINDUA ALBAM YAKE YA "HAKUNA MWANAMKE MMBAYA"

Stella Joel ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na pia ni Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA). Huduma ya uimbaji alianza muda mrefu sana, na Mungu amemuwezesha kupata kibali mbele za waimbaji wenzake kwa kuwashirikisha katika albamu yake hii  ambayo inakwenda kuzinduliwa hivi karibuni.

Stella Joel

Mungu anamtumia kwa njia ya pekee mwimbaji huyu. Watu wengi wamepata baraka kutoka kwa Mungu kwa kupitia uimbaji wake. Nyimbo zake zinagusa na zinaleta uwepo wa Mungu usikiapo. Dada huyu amefanyika baraka hata kwa waimbaji wenzake kwa kuwasidia katika mambo mengi ya kimuziki. Matamasha mengi ya waimbaji yanayofanyika hapa DSM na hata nje ya DSM, Stella Joel amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia hasa kuwatafutia wageni rasmi. Ukiangali tamasha la Ibrahim Sanga, Mess Jacob Chengula, Dr. Mage (Morogoro) na mengine mengi.
http://www.bongocinema.com/images/products/stella_joel_hakuna_mwanamke_mbaya_cd.jpg
Waimbaji wa watu wote Tanzania sasa ni wakati wa kumuunga mkono dada Stella Joel kwa kufika katika tamasha lake hili la kumshukuru Mungu na kuzindua albamu yake. Hakika Mungu atakwenda kusema na wewe siku hiyo ya tamasha.

Hivi sasa mwimbaji Stella Joel anakwenda kuzindua albamu yake ya "Hakuna Mwanamke Mbaya" katika Kanisa la KKKT Mabibo External Dar es Salaam, tamasha litakuwa siku ya Jumapili 09/11/2014 kuanzia saa 7:00 mchana na kuendelea. Mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Igunda Tabora, Mh. Dalali Kafumo.

Tamasha hili litasindikizwa na waimbaji wengi sana, baadhi yao ni Mbunge wa Singida Mh. Martha Mlata, Upendo Kilahiro, Jeni Misso, Christina Matai, Addo Novemba, Solomon Mkubwa, Ann Annie, Flora Mbasha, Mess Chengula, Ibrahim Sanga, Veneranda Bugeraha, Faraja Ntaboba, Happy Kamili, Tusi Mwanji, Joshua Makondeko, Upendo Nkone, Sifa John, Tumaini Njole, Deogras Pius (DP ), Yeronimo Mwalo, Ammy Mwakitalu na wengine wengu wakakuwepo.

Unaombwa sana kutokosa siku hiyo ya kumtukuza Mungu na kumsifu. Tambua unapokuja unakuja kumsifu Mungu ukishirikiana na wenzako, na Mungu atakwenda kukubariki kama utasifu siku hiyo kutoka moyoni ukiungana na dada wa Yesu Stella Joel.

Mimi nikutakie siku njema, ninaamini siku hiyo utakuwepo na jina la Bwana litainuliwa. Mungu akubariki sana

Comments