RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UNGANA NA VENERANDA BUGERAHA KUWATIA MOYO YATIMA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Veneranda Bugeraha ambaye ameamua  kushirikiana na watoto  yatima katika tamasha lake kubwa la kuzindua albam yake ya Ametenda. Unaombwa sana kuungana naye kwa kufika katika eneo la tukio ukiwa umebeba chochote kwaajili ya hawa watoto yatima ambao wanauhitaji mkubwa wa vitu mbalimbali.

Mnaombwa sana wachungaji, manabii, walimu, waimbaji, wainjilisti mapadre kutokosa siku hiyo, ni muda mzuri sana wa kuweza kuongea na hawa watoto yatima na wao watafarijika sana kuona wewe umeacha kazi zako na kuungana nao. Pia utaweza kuwaomba watoto hawa ili wasiangamizwe na nguvu za shetani na pia kuwaombea afya njema na mafanikio katika maisha yao ya sasa na ya baadae.

Mungu atakubariki sana mtumishi wa Mungu. Usikose kabisa, na ikiwezekana mjulishe na rafiki yako au ndugu yako ili siku hiyo kuwe na watu wengi kwaajili ya hawa watoto yatima.


Comments