RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HATIMAYE EDSON MWASABWITE KUZINDUA DVD YAKE ASILIMIA 100 MUNGU AMENIHURUMIA NDANI YA KANISA LA K.K.K.T SINZA KUMEKUCHA DAR

Mwandishi na Picha: Rumafrica

Rumafrica inapenda kukupa baadhi ya matukio yaliyotokea katika tamasha la Edson Mwasabwite katika uzinduzi wa albamu yake uliyofanyika siku ya Jumapili 07.12.2014 katika kanisa la K.K.K.T Sinza Kumekucha Dar es Salaam Tanzania


Kulia ni Mh. Martha Mlata akifuatia na Mgeni Rasmi Mh. Mama Tunu Pinda  akisaini baada ya kuingia kanisani kwaajili ya Tamasha
Leo nataka nikuonyesha kipengelea ambacho kilimhusu sana Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Tunu Pinda na mgeni mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mh Martha Malata.

Mh. Mama Tunu Pinda aliweza kuizindua albamu ya Edson Mwasabwite inayoenda kwa jina la "Asilimia 100 Mungu amenihurumia". Mama Tunu alionekana kuguswa sana na maisha ya Edson Mwasabwite ambaye ameishi katika maisha ya uyatima tangia akiwa mtoto mdogo sana.

Kutokana na maisha aliyopitia Edson Mwasabwite aliweza kusema katika mapato yake atakayopata atajitahidi kuwasaidia watoto wanaopitia maiasha aliyopitia yeye (yatima) kwani anatambua mtu kukosa mapenzi yababa na mama na jinsi mtu huyu anavyonyanyasika na hana pa kukimbilia.

Kulia ni Mh. Martha Mlata akifuatia na Mgeni Rasmi Mh. Mama Tunu Pinda
Tamasha hili lilihudhuriwa na watu wengi sana ambao walioneka kufurahishwa sana na uimbaji uliokuwa ukiendelea mahali pale. Baadhi ya waimbaji walioimba ni  Madam Ruti, Lilian, Joyce Ombeni, Beatrice Mwaipaja, Mess Chengula, Kwaya ya kanisa la KKKT Sinza Kumekucha, Emmanuel Mabisa, Addo Novemba, Stella Joel, Yeronimo Mwalo, Jane Misso, Tumaini Njole, Faraja Ntaboba, Evelyn wa Komandoo wa Yesu na wengine wengi.

Tunamshukuru Mungu kwa kuwawezesha watu kuweza kununua albamu zilizokuwa zinanadiwa na mgeni rasmi. Watu wengi walionekana kutii na kununua hizo albamu hiyo bila ya kujali kiasi kilichokuwa kikitajwa.
Mwimbaji Mkongwe wa Nyimbo za Injili Tanzania (kushoto) Jane Miso akiweka mambo safi kwa mgeni rasmi Mh. Mama Tunu Pinda

Mh. Martha Mlata kama kawaida yake na wema wake alionao kwa waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, aliweza kuchangia kile kiasi alichobarikiwa na Mungu kwaajili ya kuunga mkono maono ya Edson Mwasabwite ya kusaidia watoto yatima. Kwa yule asiyemjua Mh Martha Mlata katika Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, yeye ni mlezi wa chama hicho ni ni mmoja wa wabeba maono ya kuanzisha chama hiki ambacho kimekuwa msaada wa waimabaji wengi sana Tanzania.

Katika tamasha hili la kipekee baadhi ya viongozi wa Chama Cha Muziki waliweza kuongea machache juu ya tamasha hili na pia kuhusu Chama cha Muziki wa Injili Tanzania.

Tukianza na Mlezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Taifa, Mh. Martha Mlata Mbunge Viti Maalum CCM Mkoa wa Singida, alikuwa na haya ya kusema, "Nataka kusema kwamba, Edson Mwasabwite amepata bahati ya kutembelewa na Mgeni Rasmi Mh. Mama Pinda, ambaye mama huyu amekuwa ni mama wa huruma sana, nilipokwenda kueleza habari za Yesu alionekana mwenye furaha sana na aliweza kukubali mwaliko huu wa leo. Mbali na hayo yote, leo hii alikuwa na kazi nzito sana katika kanisa la PTA Sababsaba ambako kulikuwa na kwaya ambajyo ilikuwa inazindua leo. Lakini Mungu bado amemuwezesha kufika mahali hapa
Mh. Martha Mlata (katikati) na kulia ni Edson Mwasabwite
Katika wimbo wako Edson Mwasabwite unaosema "Umenihurumia asilimia 100" ni kweli kabisa kwa umekuwa ukijisogeza katika uso wake Mungu kwa unyenyekevu, ulitafuta uso wa Mungu na Yeye akakubariki, umeweza kuchagua njia iliyosahihi ya kumtumikia Mungu na ukaacha kwenda kule wanakoimba ndombolo ya solo lakini wewe ukasema nitakaa miguu pa Mungu na kukutumikia kwani wewe ndiye uliyenitoa utotoni na kuweza kufika mahali hapa ulipofika. Kwa kweli Mungu azidi kukubariki na kukutumia na kukupa yale yote ambayo wewe ni hitaji la moyo wako.

Ndugu zangu, Chama cha Muziki wa Injili Tanzania nataka kukisifu na kukipongeza kwa umoja walionao, waliweza kufunga safari na kufika kikijini kwangu Ushora Kibaya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida ambako kuna vumbi sana lakini waliweza kuvumilia na kufanya kazi ya Mungu. Kuna dada Tumaini Njole aliweza hata kugalagala chini kwa kucheza bila ya kujali kwamba anachafuka ila alikuwa akimtumukuza huyu Mungu aliyemuumba.

Na mwisho nataka kukushuku kanisa na wachungaji mliokubali kijana huyu Edson Mwasabwite kuja kufanyia tamasha lake hapa, Mungu awabariki sana na endeleeni kufanya hivyo na kwa wengini. Hata Mungu alisema, "Nendeni hata mwisho wa bahari mkaihubiri Injili" Leo hii Edson Mwasabwite anazindua albamu hii hapa lakini kuna watu wataenda kusikiliza majumbani mwao na kubarikiwa, na nyimbo hizi zitafika hata huko China hata kama hawajui Kiswahili ila watajua tu kuwa Yesu anatajwa na wataokoka.

Pia niwapongeze ndugu zangu mliofika, kufika kwenu sio bure, Mungu mwenyewe alijua utafika hapa na utapokea uponyaji na kubarikiwa kwa njia ya uimbaji. Kwanza nataka niwaeleze, maneno ya Mungu yanaponya hata kama hujatamka, Neno unalosikia kutoka kwa watumishi wako likiingia ndani yako basi nafsi yako inapona. Mungu awabariki sana."



Baada ya hapo Katibu Mwenezi wa Chama ChamMuziki wa Injili Tanzania, Stella Joel, naye alikuwa na haya ya kusema, "Leo hii tamasha hili limefana sana ni kutokana na juhudi za chama na pia Edson Mwasabwite ni mwanachama wa cha hiki na ndio maana unaona leo viongozi kutoka serikali, walezi wa chama wameweza kukusanyika katika tamasha lake hili.
Katibu Mwenezi Taifa wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel (kushoto)

Kwahiyo sisi tunakukaribisha sana katika chama hiki kwa lengo letu ni kuhakikisha waimbaji wa Injili wananufaika na kazi zao na hawaibiwi na kudhurumiwa, haki zao zinalindwa na chama hiki. Pia ninamshukuru sana Mh. Martha Mlata kwa kupitia yeye sisi waimbaji tuliweza kualikwa bungeni na leo hii tumeweza kumpata Mama yetu mpendwa kama mgeni rasmi wa Tamasha hili Mh. Mama Pinda. Mungu awabariki sana"

KIPINDI CHA KUCHEZA NA MGENI RASMI KABLA YA UZINDUZI KUFANYIKA




KIPINDI CHA KUZINDUA KAZI YA EDSON MWASABWITE
 Mgeni Rasmi Mama Tunu Pinda akizindua kazi ya Edson Mwasabwite
 Mgeni rasmi mama Tunu Pinda akiongea jambo juu ya Uchangishaji na Edson Mwasabwite
  Mdau wa Edson Mwasabwite akiahidi kumchangia Edson mbele wa Mh. Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) na na anayefuatia ni Mh. Mama Tunu Pinda
 Mdau wa Edson Mwasabwite akiahidi kumchangia Edson mbele wa Mh. Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) na Mama Tunu Pinda (kulia)
 Mama Tunu Pinda (kulia) akimkabidhi mdau wa Edson DVD
 Mh. Martha Mlata (wa tatu kutoka kulia) akimkaribisha mwimbaji wa nyimbo za Injili Jane Miso kutoa mchango wake. Kutoka kulia ni Mtangazaji wa Channel Ten na MC wa leo, Bwana Bony Magupa akifuatiwa na Mh.Mama Tunu Pinda
Mwimbaji wa nyimbo za injili Joyce Ombeni akitoa mchango wake




Mgeni Rasmi Mh. Mama Tunu Pinda (mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) akisalimiana na Edson Mwasabwite baada ya kuwasili kansani


Edson Mwasabwite


Dada akisoma risala ya Edson Mwasabwite

 Kutoka kulia ni mwimbaji wa gospel Emmanuel Mabisa, Katibu Mwenezi wa CHAMUITA Stella Joel, Rais wa CHAMUITA Addo Novemba
 Mh. Martha Mlata (kushoto) na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Tumaini Njole
 Kutoka kushoto ni John Shabani, Addo Novemba, Stella Joel, MC wa tamasha hili

 John Shabani (kushoto) akizungumzia umuhimu wa kujiunga na CHAMUITA


Mh. Martha Mlata akimzungumzia Edson Mwasabwite jinsi anavyomjua na pia akizungumzia faida za kuwa mwananchama wa CHAMUITA
 Mh. Martha Mlata akimzungumzia Edson Mwasabwite jinsi anavyomjua na pia akizungumzia faida za kuwa mwananchama wa CHAMUITA
  Mh. Martha Mlata
  Mh. Martha Mlata
  Mh. Martha Mlata
  Mh. Martha Mlata
  Mh. Martha Mlata
  Mh. Martha Mlata

KIPINDI CHA KUZINDUA ALBAMU YA EDSON MWASABWITE






KIPINDI CHA KUUZA AU KUNADI ALBAM YA EDSON MWASABWITE

 Joyce Ombeni na Lilian (kushoto)
 Mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bupe Kingu (kushoto)


 Edson Mwasabwite (kulia) akisikiliza maneno ya busara kutoka kwa mpenzi wa nyimbo zake mwenye asili ya watu wa Mbeya ambako Edson anatoka. Alimsihi Edson Mwasabwite kwenda kijijini kuwaimbia wanakijiji kwani wanateseka na UKIMWI na matatizo mbalimbali.






Edson Mwasabwite (kushoto)

Comments