RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ROSE MUHANDO AELEZA ALIVYOBAKWA NA RAFIKI YAKE...



SIJUI kama umeyasikia ya hivi sasa yake Rose Muhando. Na kama hujui basi mwanamuziki huyo maarufu wa kete za injili kutoka Tanzania, amefunguka mazito akisema kuwa aliwahi kubakwa.

Nyota huyo wa Bongo akifanya mahojiano na gazeti la Amani la Tanzania hivi majuzi, alisema kuwa yule aliyemtendea unyama huo alikuwa ni mtu wa karibu sana naye.

“Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye. Huyu bwana, ana jina kubwa sana Dodoma. Alinichukua kwenye gari kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana alikuwa ananisaidia katika kazi zangu,” alitanguliza.

“Nilishangaa kumuona anapeleka gari nje ya mji, nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajua. Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, naamini walikuwa wasaidizi wake”.

“Wale watu wakaniweka chini ya ulinzi na kunifunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola, nami nikasalimu amri na wakanitendea unyama huo wa kunilazimisha mapenzi” alisema Rose huku akisisitiza ni tukio ambalo hawezi kulisahau.

Licha ya kuwa alipiga ripoti polisi, Muhando amedai kuwa anaogopa kuanika jina la mbakaji huyo waziwazi kwani anahofia usalama wake kwa sababu ni mtu mwenye ushawishi mkubwa.

Comments