RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UZINDUZI WA DVD YA SEMA NA YESU NA AUDIO CD YA MUNGU ANAWEZA YA TUMAINI NJOLE WAFANA KATIKA KANISA LA K.K.K.T SINZA KUMEKUCHA

Uzinduzi ambao ulionekana kukonga mioyo ya walio wengi waliofika katika kanisa la K.K.K.T Sinza Kumekucha hapa jijini Dar es Salaam ambapo mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Tumaini Njole alipokuwa akizindua DVD yake ya Sema na Yesu na  Audio CD yake ambayo ni toleo jipya (Vol.2) inayoitwa Mungu Anaweza.
Tumaini Njole akielekea madhabahuni kwaajili ya uzinduzi

Kitu kilichowashangaza wengi ni pale tu Tumaini alipokuwa akiingia madhabahuni kwa kuimba nyimbo za kuabudu ambazo ziliwagusa walio wengi  na baadhi ya watu waliweza kutokwa na machozi. Hakika Tumaini Njole ni mwimbaji wa tofauti sana kiuimbaji na hata anavyoweza kucheza.
Tumaini Njole akiingia madhabahuni kwa kuimba nyimbo za kuabudu

Tamasha hili la uzinduzili lilihudhuriwa na waimbaji wengi sana kama utakavyowaona katika picha hapo chini. Na pia kulikuwa na viongozi kutoka serikalini kama Mh. Martha Mlata (Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Singida ) ambaye aliweza alimuwakilisha mgeni rasmi,  Mh. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha hili.
Tumaini Njole

Kwa watu wasiomjua Tuamini Njole, huyu ni mwimbaji wa nyimbo za injili  maarufu sana hapa nchini Tanzania, kipindi cha nyuma aliweza kuwa stage show malikia wa muziki wa injili Tanzania Rose Muhando kwa kipindi kirefu, lakini baadae mwenyezi Mungu aliweza kumpa karama ya uimbaji na kuwa mwimbaji wa kujitegemea.
Tumaini Njole

Tumaini Njole amekuwa nyota na asali kwa walio wengi kwani amekuwa akialikwa kwenye mikutano na matamasha mbalimbali kwa kazi ya Mungu na pia watumishi wa Mungu wamekuwa wakimtumia sana katika makongamano yao. Hii inatokana na jinsi mwimbaji huyu anavyojituma kufanya kazi ya Mungu na pengine kujinyima hata kufanya mambo yake na badala yake kutumia muda mwingi kwa kazi ya Mungu.
Tumaini Njole

Watu wengi wametokea kubarikiwa na kazi zake za uimbaji na inafika kipindi watu wanatamani hata kugusa mavazi yake wakati akiimba ili mradi tu wabarikiwe na zile nguvu za Mungu zilizomo ndani yake. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutupa mwimbaji bora na mwenye bidii katika kuinua imani za watu kwa njia ya uimbaji.
Mbali na uimbaji, Tumaini Njole ni mwinjilisti mzuri sana, amekuwa akifanya kazi hii ya uinjilisti hasa pale anapopata bahati ya kuhudhuria baadhi ya mikutano iliyoandaliwa na watumishi wa Mungu. Kabla ya kuimba Tumaini Njole huanza kwa kutoa maneno mazuri sana kwa wapenzi wake kwa kuwafundishaNeno al Mungu.
Kuna mambo mengi yakuzungumza juu ya huyu mwimbaji Tumaini Njole, tutatafuta muda na utaweza kumsikia kwa kupitia RUMAFRICA Online TV.

Tumaini Njole

Tumaini Njole



KIPINDI CHA KUKABIDHI RISALA KWA MGENI RASMI MH. MARTHA MLATA
 Katibu Mwenezi wa Chama Cha Muziki Tanzania Stella Joel akimkabidhi mwakilishi wa mgeni rasmi, Mh. Martha Mlata ambaye pia ni mlezi wa chama hicho risala ya Tumaini Njole baada ya kusomwa
 Mgeni Rasmi Mh. Martha (kulia) Mlata akihifadhi risala ya Tumaini Njole baada ya kuisoma

KIPINDI CHA KUZINDUA DVD NA AUDIO YA TUMAINI NJOLE
 Mh. Martha Mlata akionge machache kabla ya kuanza zoezi la uzinduzi
 Mchungaji wa kanisa hili la KKKT Sinza Kumekucha (kushoto) akiombea DVD na Audio CD ya Tumaini Njole na kiweka wakfu


 Mh. Martha Mlata akionyesha Audio CD baada ya kukata utepe. Upande wa kulia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Furaha Isaya




KIPINDI CHA KUNADI DVD NA AUDIO CD YA TUMAINI NJOLE
Baadhi ya wimbaji wa nyimbo za Injili waliojitokeza kununua DVD na Audio CD ya Tumaini Njole
 Furaha Isaya (kushoto) akiwa ameshika DVD na Audio CD tayari kuwagawia waimbaji kumuunga mkono Tumaini Njole
 Ndugu yake na Mh. Martha Mlata wa pili kutoka kulia akipokea DVD
 Edson Mwasabwite akipokea Audio CD ya Tumani Njole kutoka kwa Furaha Isaya
Kutoka kushoto ni Leah, Upendo Nkone, Neema Mwaipopo na Mh. Martha Mlata, wote ni waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
Mch. Lucy Wilson akitoa ahadi yake ya kumchangia Tumaini Njole

Mwimbaji Lilian Kimola (kushoto) akimwandika jina Leah baada ya kuahidi kumchangia Tumani Njole
BAADHI YA WAIMBAJIWA NYIMBO ZA INJILI WALIOMBEA

 Madam Ruti
 Silas Mbise (mwenye suti)
 Sials Mbise

Christopher (kushoto)
 Upendo Nkone (kushoto) na Mh. Martha Mlata
 Judy Sanga (kushoto) na Jessica Sanga wa pili kutoka kushoto
 Mh. Martha Mlata akimtunza Upendo Nkone wakati akiimba


Ammy Mwakitalu wa tatu kutoka kulia akimuimbia Mungu wake
 Edson Mwasabwite alivyoweza kuwa moto katika tamasha la Tumaini Njole


ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO


MATUKIO MENGINE YALIYOTOKEA KATIKA TAMASHA LA TUMAINI NJOLE



























































Comments