RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EFATHA MWENGE-UJUMBE WA JUMAPILI IBADANI ULIKUWA "UWE NA BIDII KATIKA KAZI ZAKO ZOTE ILI UWE MMOJAWAPO KATIKA MTEMBEO WA MUNGU

Mwandishi Rumafrica +255 715 851 523
Rumafrica ilibahatika kufika katika kanisa la EFATHA MWENGE kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira, na ilipofika hapo iliweza kujifunza mengi sana. Baada ya kujifunza ikaona ni vyema ikakushirikisha na wewe ambaye ulikuwa kanisani kwako au hukuweza kufika kanisani kutokana na jaribu ulilokuwa unapitia. Ujumbe wa Jumapili hii hakutolewa na Mtume na Nabii Josephate Mwingira ila ulitolewa na Mchungaji wa Eneo la Sayuni Mchungaji Aimana Dominick. Sasa ngoja ujifunze haya ambayo tumekuletea hapo ulipo.

 Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akisikiliza Neno katika Ibada ya Pili iliyoongozwa na Mchungaji wa Eneo la Sayuni Mchungaji Aimana Dominick

 Uwe mtu wa kufanya kazi kwa bidii vinginevyo utakuwa mbali na mtembeo wa Mungu. Ili uweze kutembea katika mtembeo huu lazika uwe kama askari wa jeshi la kanisa la Efatha. Katika nafasi yako fanya majukumu yako ili utembee katika mtembeo wako ili ufanikiwe. Ofisini kwako fanya kwa bidii ili watu waseme anafanya kwa bidiim na bidii zako zilete matunda mema, kwa mfano kiwa ni wakati wa kuimba basi imba kwa bidii, ikiwa ni wakati matoleo basi toa kwa bidii kwa kumtolea Mungu kilicho chema, ikiwa ni wakati wa kuhubiri basi hubiri kwa bidii kama hautahubiri tena n.k, fanya  kila kitu kwa bidii na sio kwa ulegevu.

Ukisoma Methali 22:29, ukiwa na bidii katika kazi zako utapata kibali cha kusimama mbele ya wafalme kwasababu wafalme hawa wameona juhudi zako na jinsi unavyojituma kufanya kazi yako kwa bidii. Mungu naye hutoa kibali cha kukubalika na jamii kulingana na juhudi zako za utendaji kazi.

 Mama Eliakunda Mwingira ibadani

- Wafalme 1:11:28, ukifanya maagizo kwyanayotolewa ndani ya Kanisa la Efatha, na ukifanya kwa bidii utapewa thawabu yako. Kanisa linapenda kuona watu wake ni watu wa kufanya kila jambo kwa bidii. Kama ni mchungaji, askofu, kiongozi wa kwaya, mwanazoni, mtu wa media na sehemu mbalimbali hapa kanisani, basi fanya kazi yako kwa uaminifu na kwa bidii.

Unatakiwa kujiuliza, Je, maagizo uliyopewa mwaka, umefanya kwa bidii na kiasi gani umefanya tangia Januari hii ya mwaka huu? Kama huajafanya kwa bidii maagizo uliyopewa basi anza sasa kufanya kwa bidii ili uweze kupata thawabu zako. Uwe na bidii kwa kila jambo unalofanya, ukifanya kwa bidii ile roho ya uwezesho itakujia.

Tunatamani kukuona wewe ulivyo unaonyesha kuwa umebeba habari njema. Habari hizi umezibeba na unahakikisha unazifanyia kazi kwa bidii, unajituma kuzitangaza habari njema  kwa mataifa yote kwa bidii. Usije ukawa na habari njema halafu ukazifungia katika sanduku lako. Watu wengi sana wamesahau kusona Neno la Mungu na wanashindwa hata kumtangaza Kristo kutona na kutolijua Neno la Mungu. Wengine wanatamani kumtangaza Kristo lakini wanashindwa kwasababu hawa Neno ndani yao.

Watumishi wa Mungu wakiwa ibadani wakifuatilia kwa makini maagizo kutoka madhabahuni


Natamani kukuambia jambo moja, ukiona watu wanakutuma sana basi fanya kwa bidii kwasababu wameomba unafanya kwa bidii. Watu hawa wamejaribu kutafuta mtu mwingine wa kufanya kazi hiyo wanayotaka wakutumie wewe, lakini wameona hawataweza na ndio maana wakakuchagua wewe ufanye kwasababu unafaa. Kwahiyo usione kama wanakuonea ila wameheshimu sana utendaji wako


Jaribu kumwambia Bwana, kila jambo unalotaka kulifanya  basi lifanyike kwa bidii. Kuna watu wengii sana wanatamani kufanya jambo fulani lakini wanabakia kushindwa kutokana na uvivu wao. Mungu amempa kila mtu jambo la kufanya hapa duniani ili uweze kujipatia kipato, ila kinachotutofautisha ni jinsi gani mtu anaweza kulifanyia jambo lake kwa bidii. Juhudi zako na bidii zako ndizo zitakufanya wewe uonekane wa tofauti sana na mwingine kimaisha

 Kama utafanya kazi yako kwa bidii basi Bwana atashusha Malaika wake kwako. Ili Bwana aachie zile Baraka zake kwako, basi fanya kazi kwa bidii.  Methali 10:4, afanyae kazi kwa bidii atakuwa na utajiri, na afanyae kazi kwa mkono mlegevu atakuwa maskini.

Kufanya kwa bidii kuna maumivu, kwa hiyo kunahitaji uvumilivu. Jinsi unavyojibidiisha kufanya kazi ndipo maongezeko ya kuchoka yanaongezeka. Mbali na kuchoka hata vikwazo katika maendeleo yako vinaongezeka. Sio kila mtu anatamani kukuona wewe unafanikiwa kutokana na bidii zako, watu wengi wanatamani sana kukuona kila kunapo pambazuka unazidi kurudi  nyuma. Huu sio mpango wa Mungu kabisa, tunachotakiwa ni kusimama imara katika imani zetu na kufanya kila jambo kwa bidii.

Kwa mfano mama akiwa leba hufanya kazi yake kwa bidii ili apate mtoto. Kama mama huyu hatasukuma mtoto wake ndani ya tumbo lake basi hataweza kupata mtoto na uchungu utabaki kumtesa. Kwa hiyo ili uepukane na mateso hayo yote ni wewe kufanya kazi kwa bidii.  Mhubiri 9:10, Roho saba ziko kwa wale tu wanaofanya kazi zao kwa bidii, na ukifanya hivyo utaona mafanikio.

Watu waliofanya kazi na wakapata kile walichokipata kutokana na kazi yao

(a) Mathayo 25:14-30 Inawezekana una talanta umepewa, na badala ya kuzalisha unafukia chini. Kuna watu wanamuhitaji Yesu, lakini wanapotea kwasababu wewe hufanyi kwa bidii kuwaokoa hao watu. Mpango wa Mungu ni kuona watu wanaongezeka. Watu wenye bidii wanafanya vema, wanakuwa watumwa kwa uaminifu. Unatakiwa kufanya vema katika matoleo yako ili uzidi kubarikiwa, watu wanapeleka fedha kwa Bwana zimefinyangwa sana na kukunjwa mno, mbona benki pesa hazikunjwi? Fungu la kumi ni asilimia kumi ya chochote ulichopata, je unatoa kwa uaminifu? Ukiwa mwaminifu kwa machache atakufanya mwingi wa vingi (utapata vingi). Mtumwa mwema atazawadiwa kwa mengi kwasababu amefanya vema na amefanyika furaha kwa mkubwa wako unayemtumikia.  Fanyika furaha kwa Yule aliye juu yako ili akupongeze.  Ili neno lolote likitoka madhabahuni na likudondokee, basi fanya wajibu wako kwa bidii.
Ukifanya kwa bidii Roho wa Mungu atakusaidia.

 (b) Mathayo 25:28. Ukifanya kwa ulegevu na kile ulichonacho atanyang’anywa. Chochote unachotaka kipo kwa huyo mtumishi wako ambaye anatumiwa na Mungu. Mwenye bidii akija Kanisani anahakikisha anajiweka msafi kiroho ili safari yake iwe salama. Mtu huyu hupenda kupokea kilichokisafi kutoka kwa Bwana.Itakusaidia nini kama unafanya huduma yako kwa ulegevu na siku ya mwisho ukakosa hicho kidogo na pengine kukosa ufalme wa mbinguni.

NB: Ili uweze kutoka katika umaskini uwe mtoaji ili chochote unachokifanya kwa bidii kiwe na mafanikio Fanya yale ambayo yataleta utukufu kwa Bwana.

USHUHUDA
Naitwa Felista Benjamini, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kujifungua bila upasaji, ilikua si rahisi lakini kwa neema yake Mungu wakati wakujifungua ulipofika niliambiwa njia haionekani japokuwa mtoto alikuwa kageuka kwa ajili ya kutoka haikuwezekana kwani njia ilikuwa haionekani. Ikabidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili, nilipofika daktari wa kunifanyia upasuaji hakuwepo, alikuwa kufanya upasuaji kwa mtu mwingine.

Mimi sikuacha kuomba nikimsihi Mungu nikamwambia Mungu kama Mama Maria(Yesu) alijifungua kwa upasuaji, basi na mimi nitajifungua kwa upasuaji. Kama Maria(Yesu) alijifungua kwa kuongezewa njia basi na mimi nitaongezewa, baada ya kusema na Mungu, ilikuwa kama muujiza kwangu nilimwambia Mungu kwamba mtoto anatakiwa atokee sehemu aliyoingilia.

Basi niliendelea kumsihi Mungu kwa hilo baadaye nilipofikia zamu yangu kuingizwa chumba cha upasuaji nilimwambia Mungu nakuomba unipe nguvu ya kusukuma kwani Roho wa Bwana yu juu yangu! basi nilijikuta Napata nguvu ya ajabu nikasukuma na mtoto akatoka walishangaa kuona vile, lakini najua kwa kuwa huu ni mwaka wangu wa Mtembeo wa Mungu basi Mungu hakuniacha peke yangu Amina.










Comments