RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM: SOMO LA JUMAPILI LINASEMA "MWAKA WA KUTEMBEA NA BWANA"


Rumafrica ilibahatika kufika kantika kanisa la Efatha Mwenge na kuweza kuhudhuria Ibada ya Jumapili ya terehe 4/1/2015 ya saa 4:00 Asubuhi. Katika Ibada hiyo Nabii na Mtume Josepahte Mwingira hakuweza kuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kihuduma na badala yake kulikiuwa na mhubiri ambaye Rumafrica haikubahatika kupata jina lake. Muhubiri huyu aliweza kutufundisha somo kama linavyoojieleza hapo chini:

Nabii na Mtume Josephate Mwingira mwanzilishi wa huduma ya Efatha (Funguka)duniani.


SOMO: MUNGU ANA MPANGO NA WEWE
GOD HAS SPECIAL PLAN FOR YOU
Kwa waumini wa Efatha mwaka huu ni mwaka mzuri kwao wa kutembelewa na Mungu. Kwa hiyo tunahitajika kuwa na mambo yafuatayo:
1.       1. Nidhamu ya Kiroho
Mungu hakutembea na watu wengi bali aliweza kuchagua taifa la Israel kutembea nalo kwasababu alikuwa na mpango nalo. Leo hii Mungu amechagua kanisa la Efatha kutembea nalo
KWANINI MUNGU ANA MPANGO NA SISI?
Mungu hufanya kazi na wale wampendao. Sio jamii yote ya Waafrika Mungu ana mpango nayo au anatembea nayo ila kuna baadhi ya jamii Mungu anatembea nayo na hasa ile inayompenda. Ipo jamii ambayo inamjua Mungu na ukiangalia kiundani utaona maisha yao ni mepesi. Kuna familia zingine zimepewa kibali cha kuwasaidia wengine au familia zingine zenye kuteseka na hizo familia ndizo tunazosema maisha yao ni mepesi na zinajitahidi kufanya familia zingine zenye maisha magumu kuwa mepesi. Watu walioitwa ndani ya kusudi la Mungu watapatiwa mema.

AINA YA MAKUNDI AMBAYO MUNGU ANA MPANGO NAYO.
(a) Walio mtelekeza Mungu
(Warumi 8:28, Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake). Hawa ni watu waliomfahamu Mungu lakini wakafika mahali wakamkataa Mungu. Usifike sehemu ukamtelekeza Mungu

     (b)  Waliokubali (Isaya 1:19
Mungu anasema kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi. Kitu unachotakiwa kufanya ni kukubali ufahamu wa Mungu na kukaa ndani yake. Mungu ana mpango na wewe siku ya leo. Sisi tumepewa kufahamu ufahamu wa Mungu kwa kusoma Neno lake (Biblia) na kurudia yale tuliojifunza kanisani na watumishi wa Mungu. Bwana anasema, “Nasi twajua katika mambo yote na hao wampendao watakula mema ya Mungu”
MUNGU ANAMPANGO GANI KWETU?
      (a)      Kukuinua katika nafasi ya juu. (To take you to your highest level) (Hagai 2:9
Mungu anasubiri uumbe jambo jipya katika ufahamu wako. Mungu ameweka mpango katika ratiba yake kuwa Yule aliyemkubali atamwinua kutoka chini na kuwa juu. Kwa mfano: Umetoka nyumbani kwako ambako unaamini hakuna utukufu ukilinganisha na kanisani, ukaja kanisani ambako kuna utukufu mkuu kuliko nyumbani kwako, kutokana na imani yako hiyo ya kuamini kuwa kanisani kuna utukufu basi amini ya kuwa utainuliwa kuwa juu kwasababu umeingia mahali patakatifu. Hautakiwi  kuchafua utumishi wako, linda sana huduma yako isichafuliwe na usiichafue.

      (b)     Kukupa Kibali mara dufu
Maombi yako yaendane na kanuni ya kutii yale yote unayosikia kwa mtumishi wa Mungu.
Pasipo Neno ndani yako basi tambua ya kuwa hakuna maombi yanweza kufanyika kwasababu ni mtupu ndani ya ulimwengu wa Mungu kwa ufahamu ya Mungu kwa njia ya Neno la Mungu.. Katika Neno kuna ujumbe wa Kinabii na hakuna atakayekuzuia.

           (c) Kukufikisha katika hatma yako.
Hapo ulipo anapotaka ulipo, bali pale alipo Mungu ndipo anataka uwepo. Mpango wa mwanadamu unaweza. Mpango wa mwanadamu unaweza kuwa kama udhamira ya Mungu. Mungu akikuotesha jambo usingizini basi ujue Mungu anakuonyesha kuwa utakuwa hivyo. Mpango wa Mungu na wazo la Mungu na kukuwezesha kuwa bilionea. Mpango wa Mungu kukuhakikishia usalama na katika mipango yako na kazi zako.

     (d) Kuhakikisha Usalama.
Mbaraka unahitaji kulindwa na kutukuzwa. Kwa wanaotaka kuolewa na kuoa Mungu anaenda usalama na kuhakikisha unampata mke au mume mwema kwako. Utafika wakati unatamani kutoa cheque sadaka kwa Bwana na sio 20,000/=

Comments