RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAKAZI WA TEGETA DAR UJUMBE WA MUNGU SASA UMEWAFIKIA. MTUME PETER NYAGA KUWASHA MOTO WA INJILI


Kazi ya Mungu hufanywa na walio wake, sasa ni wakati wako wewe mkazi wa Tegeta na jiji zima la Dar es Salaam kuungana na watumishi wa Mungu katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku tatu Tegeta Kibaoni. Mkutano huu ni wa kurejeshewa vile vyote ulivyonyang'anywa na shetani. Umeteseka vya kutosha, Bwana anakwenda kukupumzisha kwa kupitia watumishi wake. Lichukulie jambo hili kwa umakini ukiwa na imani kuwa Mungu anakwenda kufanya jambo katika maisha yako, anakwenda kukuokoa, kukubariki, kukufariji, kukuponya, kukuimarisha kiafya, kubariki kazi ya mikono yako.

Mtume Peter Nyaga

Mtumishi wa Mungu Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe, Nabii Isaac Nyaga kutoka Kenya na mwenyeji wa kanisa la RGC Tegeta Mch. Isaac Mwiti watahakikisha unaondoka ukiwa wa tofauti kabisa na jinsi ulivyokuja, Bwana anakwenda kuwatumia kwa njia ya ajabu sana.


Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523


Waimbaji watashusha uwepo wa Mungu kwa sifa na kuabudu siku hiyo, yaani wewe utakuwa ni mtu wa kupokea tu, iala unachotakiwa kufanya ni kujitakasa kwa damu ya Yesu Kristo na kutubu dhambi zako zote ili Mungu aweze kufanya makubwa katika maisha yako.
USIKOSE na MUNGU AKUBARIKI SANA

Comments