RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IBADA YA JUMAPILI EFATHA MWENGE: MLANGO UMEFUNGULIWA MBELE YAKO FANYA NGUVU UINGIE MAANA WAPO WAKUPINGAO

Mwandishi: Rulea Sanga +255 715 851 523
Jumapili hii Rumafrica ili bahatika kufika katika kanisa la Efatha Mwenge na kuweza kuhudhuria Ibada iliyojaa upako wa aina yake. Watu waliweza kupokea Neno la Mungu kwa kupitia Mchungaji (jina halikupatikana)na hivi ndivyo ilivyokuwa.

Mch. David Mwakisole Mchungaji kiongozi Mwenge akifundisha Neno Ibada ya pili Somo lenye Kichwa :


Wakorintho 1:16:8-9

Habari ni habari inayoonyesha mipango ya mtu kufikia malengo yake, Mungu anaweza kufanya mlango wako lakini wapo wapingao. Sisi tunaweza kuwa na malengo au mawazo lakini wapo wapingao, kuna vitu vingi vinaweza kusababisha upinzani wa malengo yako.

1. Mazingira
2. Kazi uliyonayo

Unataka kumtumikia Mungu lakini kazi yako inazuia, unakosana na Mungu. Kitu kinachosababisha hayo yote ni shetani ambaye anakupa hofu.

Unaweza kubuni mradi lakini unavyobuni kwa kuangalia Yule anayekupinga, andaa njia za kupambana na anaye kupinga. Mpinzani anaweza kuondolewa na wewe mwenyewe kwani silaha na mbinu zote unazo, umekabidhiwa na Mungu.

Luka 10:1-3
Kusudi la Yesu kwetu sisi na kwanini tunashindwa, Yesu ametuandalia mpango kwetu sisi wanafunzi wake kuwaleta kondoo kutoka kwa mbwa mwitu. Unapenda kuvuna tambua kuwa usijiamini peke yako bali amini na Yule mchungaji aliyekutuma. Wewe ni sehemu ya wavunao na unatumwa na Mungu na wapinzani wako ni wengi.

Efatha mass choir wakimsifu na kumwabudu Mungu wetu Ibadani leo.

Ni kweli tunaomba lakini tunashindwa kuwaleta watu kwa Mungu, upinzani hauwezi ukiwa umeelewa upona nani, Ukielewa kuwa una Yesu Kristo upinzani hautaweza kutokea.

Unaporaruliwa na mbwa mwitu wakati unawavuna watu wa Yesu, usikate tamaa kwa maana anayekutuma anajua hatari iliyopo mbele yako.

Wanaokupinga hawawezi kukupinga milele kwasababu unaye Yesu. Joshua 1:7-8 namna gani unaweza kumpinga adui yako?

1) Kuwa hodari
2) Kuwa na ushujaa

Ili uwe hodari na shujaa angalia nini umeangizwa na mtumishi wake Mungu, ukifanya hivyo mbele yako kuna ushindi. Tunayoagizwa madhabahuni kwa watumishi yanatupeleka kuliko kusudi la Mungu , unatakiwa kutafakari maneno ya Mungu na kuyafanyia kazi.

Omba uombavyo lakini sheria ya Mungu iwe ndani yako, tuwe tunakiri tofauti na ulimwengu ulivyo.Mtu anayeitwa kwa mpango wa Mungu, Mungu anauwezo wa kusema lolote juu ya baya lililoko mbele yako. Unavyoona matetemeko ya nchi wewe angalia uliye na uhusiano naye na sio matetemeko, tusiishi kama ulimwengu unavyosema bali Mungu anavyosema.

Pale alipo Yesu ndipo tulipo kwa hiyo tunatakiwa kuwa na ujasiri, na kwa kufanya hivyo hakuna atakaye tupinga. Biblia inasema atafutaye huona, abishaye atafunguliwa, unatakiwa kutafakari manneo ya Mungu mchana na usiku.

Mungu alileta maneno yake katika Biblia ili tuweze kubadilisha tabia, Yesu anasema mimi si wa hukumu ila maneno yangu ndiyo yatakayo wahukumu.

Kwa kushika sheria za Mungu naye anatupa nguvu ya kutimiza kusudi la kutuweka duniani. Efeso 3:20, ipo nguvu iliyowekwa ndani yetu ambayo huuwishwa baada ya kutafakari na kufuata sheria za Mungu.

Neno la Mungu ni upanga kwani katika neno la Mungu kuna nguvu ya ajabu sana. Ipo nguvu kwa kila mtu na sio kwa watu wachache, ila watu hatutambui. Nguvu itatokea pale utakaposema sasa mimi nimeamua kuwa na Yesu wakati wa kiangazi na masika. Kuna vitu ambavyo unafanya ambavyo zamani ulikuwa hufanyi, basi usikate tamaa kwa maana utafanya vikubwa zaidi ya hapo, ni wewe kukazana.

Warumi 8:28, Mungu hufanya na wale wampendao kupata mema, unapoanza kutafakari kazi ya Mungu ndipo Mungu anaanza kuwa na wewe, nguvu tunapata tunapotafakari neno la Mungu. Matendo 4:7

Sisi tumepewa jina la Yesu Kristo ambalo ni silaha yetu kubwa. Isaya 53:4-5, Bwana amechukuwa masikitiko yetu na makosa yetu, alipigwa na sisi tumepona na kujeruhiwa kwake sisi ni wzima.

SHUHUDA
AFAHULU MASOMO YAKE

Naitwa Cosmas Peter, wa eneo la Shalom, Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza chuo kikuu na kufaulu mitihani ya CPA, leo niko mbele yenu namshukuru Mungu, mwaka 2009, nilimaliza chuo kikuu huria, nilifanya mitihani yangu ya CPA lakini sikufanya vizuri masaomo yote. Baada ya hapo nilianza masomo ya kukulia wokovu, ubatizo wa maji mengi na Roho Mtakatifu. siku moja Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema , ukitaka kutoka mahali ulipo dhamiria moyoni mwako, baada ya hapo niliondoka na kutoa pesa zilizokuwa kwenye akanti yangu ya benki na kutoa madhabahuni. Baada ya kutoa hizo pesa zote miezi mitatu baadaye nilipata pesa nyingine kwaajili ya ada ya chuo, ndipo 2014 nilianza tena chuo na kufanya mitihani yangu ya CPA na kufanya vizuri masomo yote, kwahiyo ndani ya mwaka mmoja nikafanikiwa kumaliza masomo ya CPA. Hivyo namshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea. Kwa hiyo nawasihi wana wa Mungu washike neno linalotoka madhabahuni na kulitendea kazi ndipo watakapoona matokeo yake.



JOHN MASENGA (APATA UPONYAJI DHIDI YA UGONJWA WA TEZI DUME)
Leo ninatoa ushuhuda wangu nilikuwa nasumbuliwa na tezidume ambalo lilikuwa linanisumbua kwa mda mrefu madaktari walisema nifanyiwe upasuji lakini mimi na mke wangu tukasema daktari ni MUNGU hivyo tukaingia kwenye maombi, nilivyoenda kupima Daktari aliniambia sina tena tatizo hilo, yaani ni alinikuta ni Mzima kabisa hivyo namshukuru MUNGU.