RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER ALIVYOHUBIRI SIKU YA JUMANNE 24/02/2015 KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA DSM TANZANIA

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA 2 NYAKATI 20:20-22
Biblia inasema: Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa, nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama akasema, nisikieni enyi Yuda, nanyi wenyeji wa Yerusalemu, mwaminini Bwana Mungu wenu, ndivyo mtakavyo thibitika, waaminini manabii wake ndivyo mtakavyo fanikiwa; ukiamini hakuna jambo linaloshindikana, ukitamkiwa mimba na utapata mimba, nataka ufanikiwe juu ya kazi zako, juu ya kampuni yako, juu biashara zako, juu ya ndoa yako.

Nabii Flora Peter
Biblia inasema: Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakao mwimbia Bwana na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi na kusema, mshukuruni Bwana kwa maana fadhili zake ni za milele; hii ni wiki ya shukurani, tunapaswa tumshukuru Bwana, ametupigania wiki tatu, na hii ni wiki ya shukurani na maombi. Mshukuru Bwana hata kwa afya uliyonayo, hata kwa hatua uliyofikia.
 Nabii Flora Peter
Biblia inasema: Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni na wana wa Moabu; wanaovizia maisha yako watapigwa maadui zako wote, siku walipomsifu Mungu Paulo na Asila milango ya gereza ilifunguka, kumsifu Mungu kunaleta nuru.



JINSI YA KUFIKA KANISANI
Kanisa liko mkoa wa Dar es Salaam Tanzania. Panda magari ya Tegeta, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la Nabii Flora Peter. Utaona Bajaji na pikipiki nyingi hapo kituoni.

Tembelea www.nabiiflora.blogspot.comwww.nabiiflora.blogspot.com
Facebook: Nabii Flora Peter

Comments