RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA TATU ZA MESS JACOB CHENGULA AKIWA NA MCH DANIEL KULOLA - MWANZA

Mess Jacob Chengula ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Katika waimbaji ambao wameonyesha bidii katika kazi ya Mungu, hutamsahau kumtaja Mess Jacob Chengula. Mwimbaji huyu kwa muda mfupi ameweza kufahamika karibu Tanzania nzima kwa juhudi zake za kutangaza nyimbo zake kwa njia mbalimbali kama vile mitandaoni, redio na katika runingani. Mungu amempa kibali cha kukubalika na wachungaji, manabii, mitume na watumishi wa Mungu mbalimbali kutokana na uimbaji wake na heshima awapo katika kazi ya Mungu.


Mess Jacob Chengula (wa pili kutoka kulia) akifuatiliwa na Mch. Daniel Kulola

Mess Jacob Chengula ambaye kwa sasa amebahatika kutoa albamu yake ya kwanza ambayo inaenda kwa jina la MUNGU HABADILIKI. Hakika albamu hii ni nzuri sana ukianzia kuangalia video yake ambayo imechukuliwa katika sehemu mbalimbali kama vile Tanzania, China na Dubai. Hii inaonyesha ni jinsi gani mwimbaji huyu alivyotumia mali zake kufanya kazi ya Mungu kuwa ya viwango vya kimataifa.

Mbali na uimbaji pia ni mfanyabiasha katika soko kubwa Tanzania la Kariakoo. Mungu anazidi kumbariki sana. Mwimbaji huyu amekuwa katika mstari wa mbele kugawa albamu yake pale anapokuwa jukwani bure, na hii hutokana na ule moyo wa upendo kwa wadau wake. Mara nyingi hutamani sana kuona watu wanapata kusikia kazi yake ili waweze kubarikiwa ujumbe ambao anaamini amepewa na Mungu kwaajili ya kuokoa roho za watu, na hii humfanya kuamua kugawa albamu zake kwa wadau bure ili hata yule asiye na fedha aweze kupata ujumbe alipewa na Mungu.


Comments