RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FLORA PETER

DADA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEPONA UPELE

Bwana Yesu asifiwe
; nilikuwa ninamaupele, yaani nilikuwa najikuna hata kisu unaweza kuchukua na kujikuna nacho. Namshukuru Mungu baada ya kutumia sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, maupele yote yamekwisha.
SYLVIA JOHN ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMETAFUTWA NA NDUGU ZAKE WALIOPOTEZANA SIKU NYINGI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Silivia John
; juzi nilichukuwa sabuni iliyoombewa na Nabii Flora nikaiogea, muda huo huo nikatoka nikaacha simu ndani. Nilivyorudi nikakuta missed call za watu ambao nilikuwa sitegemei kabisa kama wangenipigia, na lain nilibadilisha mara mbili na namba zao sina sasa nashangaa sijui walipataje namba zangu. Baada ya hapo nikawa bip, akanipigia simu mjomba wangu ambaye tulipotezana kwa muda mrefu sana toka nikiwa naishi Uganda, akaniambia wewe ni mtoto wetu hata kama dada yetu alishakufa.
ANGELA WILLIAM AU MAMA SYLVIA ANAMSHUKURU MUNGU MWANAYE AMEPONA MAUMIVU YA MOYO BAADA YA KUMPAKA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Angela William
; namshukuru Mungu kupitia sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, mtoto wangu alinipigia simu usiku kwamba moyo unamuuma, nikachukuwa sabuni nikampaka nikasema Mungu wa Nabii Flora maumivu yote yaondoke kuanzia sasa. Namshukuru Mungu alipoamka asubuhi akasema anasikia maumivu kwa mbali kama akipumua.
SILIVIA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA MAUMIVU YA MOYO BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA PIA AMEPATA PESA ZAKE ZILIZOKUWA ZIMEPOTEA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Silivia
; ushuhuda wa kwanza ni huo alioshuhudia mama, moyo ulikuwa unaniuma lakini baada ya kupaka sabuni maumivu yakaisha. Ushuhuda wa pili, nilipotelewa na pesa kama wiki mbili zimepita, lakini jana baada ya kurudi shule nikaikuta ile pesa imekaa juu, namshukuru sana Mungu
.
JANET AMASHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA MAJI, SABUNI NA STICKER YA NABII FLORA MGONJWA ALIYEKUWA KATIKA HALI MBAYA AMEWEZA KUPONA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Janet
; jana tulienda kumwangalia mgonjwa tulipigiwa simu kuwa amefunga kauli, tulienda na maji yaliyoombewa na Nabii Flora, tukabeba sabuni pamoja na sticker. tulipofika nikachukuwa maji nikammiminia kichwani, baada ya kumwagia maji akaanza kukoroma, nikachukuwa maji tena nikampaka na sabuni na sticker tukamwekea ubavuni, akazinduka akasema alikuwa akifumba macho anasikia watu wanamwita. Lakini baada ya hapo akasema hata akifumba macho haoni tena watu wakimwita na akapata usingizi angali alikuwa hajalala siku mbili, namshukuru Mungu sasa hivi ni mzima na yupo Kanisani.
MAMA ANAMSHUKURU MUNGU MDOGO WAKE BAADA YA KUOGESHEWA STICKER YA NABII FLORA HALI YA KUKAKAMAA IMEKWISHA


Bwana Yesu asifiwe
; kupitia sticker ya Nabii Flora imemponya mdogo wangu, siku ya Ijumaa nilienda kumwangalia mdogo wangu alikua anaumwa, sasa wakati namlisha chakula akaniambia anataka kukojoa, akiwa anataka kukojoa anakakamaa mpaka mdomo unaenda pembeni. Mimi nikawa naomba kwa kutumia sticker ya Nabii Flora, nilipoondoka nikamwachia mdogo wangu hii sticker nikamwambia awe anamwogeshea mgonjwa, namshukuru Mungu mdogo wangu kanipigia simu ile hali ya kukakamaa imetoweka kabisa.

JINSI YA KUFIKA
KANISA LIPO MBEZI SALASALA DSM TANZANIA
Panda magari ya Tegeta, Shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la Nabii Flora Peter
Tembelea

Comments