RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TULIYEOKOKA TUMEPATA CHANGAMOTO NA WENZETU WA CLOUDS MEDIA KUCHANGIA DAMU

Waimbaji wa nyimbo za Injili, mablogazi, ma-designer, wachungaji, Manabii, Mitume, Maaskofu, Mapadre, Wainjilisti, Walimu  na wengine wengi hapa Tanzania tujitokezee kuchangia damu mahospitalini, wenzetu wa Bongo Fleva na Clouds Media wamechukua hatua na kuona umuhimu wa kuchangia damu. Wenzetu wanateseka mahospitalini na sisi tunaweza kuwaokoa kwa damu zetu na maombi. Tuamke sasa tuelekee mahospitalini. Hii ni kwa watu wote waliokoka wakawasaidie ndugu zetu wanaoteseka. Kutoa ni moyo na sio utajiri. Nitafurahi sana kukuona ukichukua hatua, usisubiri kiongozi wako aseme, ni wewe kufika hospitalini na kutoa damu yako kuokoa maisha ya watu. Hii habari ni pamoja na kwa mablogazi na ma-designer wote Tanzania

Wako katika Bwana
Rulea Sanga


Sehemu ya damu iliyokusanywa baada ya wananchi kuchangia.


WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam, leo walijitokeza katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya waathirika na wahitaji wa huduma hiyo.
Zoezi hilo lilifanyika katika Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Clouds Media, Hospitali ya Muhimbili, Damu Salama na wadau wengine.

Msanii wa Muziki wa Hiphop, Kala Jeremiah amewahimiza wasanii na wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi wanaoaga dunia kwa kutokuwa na damu nyingi katika ajali na kwa kina mama wajawazito.


  Msanii, Kala Jeremiah akisisitiza watu kujitokeza katika kuchangia damu.…


Msanii, Kala Jeremiah akisisitiza watu kujitokeza katika kuchangia damu.

ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI



Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Kiango akichangia damu.


Wafanyakazi wa Clouds Media wakiwa kwenye kampeni ya uchangiaji damu.

Baadhi ya wataalamu wakitoa ushauri na huduma kabla ya kuchangia damu.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni
.

Comments