RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ZIARA YA TUMAINI NJOLE ZANZIBAR YAFANYIKA BARAKA KATIKA MAISHA YAKE

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Tumaini Njole alipata mualiko wa kuhuduma katika semina ya OPARESHENI AMKA iliyoandaliwa na kanisa la K.K.K.T Mwanakwelekwe Zanzibar linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Mvungi kwa muda wa wiki moja.


Tumaini Njole akiongea na Rumafrica alisema, hakika ameona mkono wa Mungu alipokuwa akifanya huduma yake ya uimbaji,  watu wengi wametokea kumpenda sana na hii inasababishwa na ukarimu walio nao wakazi wa Zanzibar na jinsi wanavyowapenda waimbaji kutoka Tanzania Bara. Watu wengi sana waliweza kuokoka katika semina hiyo. Watu kutoka sehemu mbalimbali waliweza kufurika katika kanisa hilo na kusababisha kanisa kujaa.

Tumaini Njole kabla hajaaza safari ya Zanzibar

Mwimbaji huyu mwenye shauku ya kumtumikia Mungu wakati wa ujana wake alizidi kusema, "Mungu ni mwema jamani, watu wa Zanzibar wanampenda sana huyu Yesu tunayemtumikia, wana hamu kubwa sana ya kumjua kiundani Yesu Kristo, wanawapenda waimbaji na wamekuwa wakarimu sana kwangu, hakika nimefurahi sana kwa mapokezi yao kuanzia airport mpaka sehemu yangu ya kupumzika. Mungu azidi kuibariki Zanzibar na watu wake ili amani itawale. Nawashukuru  sana wachungaji, viongozi mbalimbali wa kanisa la K.K.K.T Zanzibar, walimu, wahudumu, waumini na wakazi wa Zanzibar na kila mmoja aliyehusika katika uwepo wake hapo Zanzibar"

Tumaini Njole amesema hata kama safari yake ya kuelekea Zanzibar ilikuwa na vikwazo hasa walipokuwakwenye ndege angani, ndege yao ilianza kuyumba kama inataka kudondoka, lakini Mungu aliwasimamia wakafika salama. Hata alipoweza kufika shetani alweza kujitokeza tena na kuweza kuzuia semina isiendelea kwani kulitokea kitu kama shoti ya umeme, vyombo vya muziki vikagoma kuwaka kwahiyo ikawapasa kutumia sauti zao kupaza sauti kwa Mungu ili afanye jambo juu ya hilo jaribu waliokuwa wakipitia.

Watumishi wa Mungu waliweza kumtembeza mtumishi wa Mungu tumaini Njole sehemu mbalimbali za Zanzibar na hasa sehemu za makumbusho kama utakavyoona katika picha.

Rumafrica inafanya jitihada za kumtafuta Tumaini Njole ili kufanya naye mahojiano juu ya ziara yake ya Zanzibar

Unaweza kuwasiliana na Tumani Njole kwa simu hii +255 716 551 269

TUMANI NJOLE AKIWA KATIKA SEMINA YA OPARESHENI AMKA SIKU YA KWANZA
 Tumaini Njole akiwasha moto wa Injili kwa njia ya uimbaji
  Tumaini Njole akisifu na kuabudu
  Tumaini Njole

TUMAINI NJOLE AKITEMBEZWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MAKUMBUSHO - ZANZIBAR
Mtumishi Jacob Mlawa kulia na Tumaini Njole
 Tumani Njole akiwa katika kanisa la kale la Anglikana, ndani ya kanisa hili kuna kaburi la mwanaharakati wa kutetea na kukomesha utumwa

Kaburi la mwanaharakati aliyekuwa akitetea na kukomesha utumwa Zanzibar

 Tumani Njole akiwa katika kanisa la kale la Anglikana, ndani ya kanisa hili kuna kaburi la mwanaharakati wa kutetea na kukomesha utumwa
 Tumaini Njole aiwa ameshika Pingu zilizokuwa zikitumika kipindi cha utumwa kuwafunga watumwa. Na hapo yuko katika eneo ambalo watumwa walikuwa wakilala, paa yake ni fupi sana

 Tumaini Njole akiwa ameshika mnyororo uliotumika kuwafunga watumwa
 Kulia ni Mtumishi Jacob Mlawa, Tumani Njole wakielekezwa sehemu mbalimbali na mwenyeji wako aliyevalia tshirt nyekundu

 Tumaini Njole akiwa katika eneo la sanamu za watumwa Zanzibar
  Tumaini Njole akimtafakari Mungu katika eneo la sanamu za watumwa Zanzibar
 Tumaini Njole akiwa katika Kanisa la kale la Anglikana Zanzibar likifanyiwa ukarabati
 Tumani Njole na mtumishi Jacob Mlawa wakiwa ndani ya kanisa la kale la Anglikana Zanzibar
 Tumani Njole akipata historia ya kanisa la kale la Anglikana
 Hii ni madhabahu ya kanisa la kale la Anglikana


TUMAINI NJOLE AKIMTUMIKIA MUNGU SIKU ILIYOFUATA HUKO ZANZIBAR

Kutoka kulia ni Mch. Mvungi, Tumani Njole na Mtumishi Jacob Mlawa
 Tumani Njole akiwa katika uwepo wa Mungu
  Tumani Njole akiwa katika uwepo wa Mungu
  Tumani Njole akiwa katika uwepo wa Mungu
  Tumani Njole akiwa katika uwepo wa Mungu




TUMAINI NJOLE AKIWA KATIKA SAFARI YA KUELEKEA DAR ES SALAAM

TUMAINI NJOLE AKIWA AMETUA KATIKA AIRPOT YA DAR ES SALAAM
 Tumaini Njole akiwa katika ardhi ya Dar es Salaam baada ya kutoka Zanzibar


 Tumaini Njole akiwa na furaha baada ya kufika salama kutoka Zanzibar


Comments