Sema Nao Bwana ni DVD ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Elizabeth Ngaiza ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana sokoni kutokana na ule mwitikio wa watu kununua na kujipatia ujumbe mzuri sana wa kumtukuza Mungu na wenye kukufariji. Kutokana na maelezo ya mwimbaji huyu amesema kwa sasa anauza DVD yake katika gari lake ambalo limewekwa label ya jina lake na jina la DVD hiyo.
Elizabeth Ngaiza -Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
Huu ni wakati wako wa kujipatia DVD hii ili ifanyike baraka katika maisha yako. Kumbuka mwimbaji huyu kabla ya wokovu alikuwa mtu wa pombe sana, lakini Mungu aliweza kumbadilisha na sasa ameokoka anamtumikia Mungu. Katika nyimbo zake kuna baadhi ya nyimbo ameimba kuhusiana na mapito aliyopitia kama vile ulevi na hasara zake. Pia ameimba baadhi ya nyimbo kwa lugha ya Kihaya ikiwa ni moja ya zawaidi kwa Wahaya na wale wanaojua Kihaya.
Elizabeth Ngaiza ambaye kwa kabila ni Muhaya na Mungu amempa neema ya kuwa daktari na pia mjasiriamali. Huu ni ushuhuda tosha sana kuwa Mungu ameweza kumtoa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Dada huyu hakuweza kukata tamaa ya kumtafuta na kumtii Mungu na baadaye akaweza kula matunda kutoka kwa Mungu na sasa amebaki kumtumikia kwa njia ya uimbaji.
DVD ya Elizabeth Ngaiza -Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
Akiongea na Rumafrica kwa njia ya simu, alisema kwa sasa yuko tayari kufanya kazi ya Mungu na wewe kama utamualika katika matamasha yako, mikutano yako, kanisani kwako, kwenye sherehe, na matukio mbalimbali, ataweza kufika na kushiriki kufanya kazi ya Mungu. Anatambua kuwa yeye ni kijana na mwenye nguvu kwahiyo ana kila sababu ya kufanya kazi ya Mungu. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu hii +255 714 294 0716

Comments