RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GWT WATIKISA JIJI LA DAR KWA KUSHUSHA UWEPO WA MUNGU NA SUNDAY CELEBRATION SEASON I...BAADA YA HAPO JUMAPILI HII WATAKUWA KATIKA UKUMBI WA VICTORIA

Siku ya Jumapili 22/03/2015 ni siku ambayo Glorious Worship Team (GWT) wameandika historia katika kitabu chao kwa kufanya tamasha la kwanza mwaka 2015 katika ukumbi tulivu wa  Ginang Restaurant Victorioa jijini Dar es Salaam.


GWT ni vijana ambao wameamua kufanya kazi ya Mungu katika kipindi chao cha ujana. Siku ya jana waliweza kuonyesha watu kuwa Mungu anaweza kuwatumia katika kutangaza Neno lake wa njia ya uimbaji. Ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya kitu kama kile, kiongozi wa GWT aliweza kutamka kuwa huo ulikuwa ni utambulisho wa matamasha yao ambayo yatakuwa yakifanyika kila Jumapili yakienda kwa jina la  GWT Sunday Celebration - Spirit of Praise.

Jumapili ya 29/03/2015 watakuwepo katika ukumbi Victoria ulilopo katika kituo cha mafuta cha Victoria barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam

Kwa wasiojua, hawa ni waimbaji wa nyimbo za Injili ambao wanatokea makanisa tofauti, na waliamua kuungana pamoja na kufanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji. Kundi hili lilianza mwaka 2011 liliitwa Glorious Celebration na sasa ni Glorious Worship Team (GWT)





Imma Base

Kutoka kulia ni Melisa John, Emmanuel Mabisa, Ester

 Wanakamati wa GWT siku hiyo: Kutoka kulia ni Naomi, Miriam, Vicky


Kulia ni Mosax


Paul Clement



The Next Level






MATUKIO MENGINE BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO



Samuel Sasali akiwa na mkewe Milembe (kulia)

















Hali



Pastor JK John Komanya akiwa na timu yake.

Pastor Sam na watoto wa Next level



Calvary Band wakifanya kweli kwenye mwendo
Fred Msungu

Tito akiwa na pacha wake…..














Comments