RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA -MWENGE: UTAKATIFU / MTAKATIFU

Rumafrica For All Nations kwa neema ya Mungu ilibahatika kuhudhuria ibada ya Jumapili 02/03/2015 katika kanisa la Efatha lililopo Mwenge Dar es Salaam Tanzania. Ibada ilikuwa njema sana kutoka na uwepo wa Mungu . Katika ibada hii tulijifunza juu ya Utakatifu au Mtakatifu na somo lilikuwa kama ifuatavyo.


UTAKATIFU/MTAKATIFU
Huu ni mwaka wa mtembeo na Bwana. Leo tutajifunza juu ya Utakatifu au Mtakatifu. Mtakatifu ni Mungu na ji jina lake. Tusome Ufunuo 4:8, Mungu anataka sisi tulio wake tuwe watakatifu kama Yeye alivyomtakatifu ili tuweze kutembea naye katika mtembeo wake.
Watakatifu walioko duniani na ndio bora na ndio Mungu aliopendezewa nao, soma Zaburi 16:3. Uwe na shauku ya kuwa matakatifu ili uwe bora hata kuliko walioko mbinguni. Popote palipo na utakatifu Mungu yupo hapo. Ukiona umefanya ibada na ukaona  hujaona uwepo wa Mungu ujue hapo hakuna Roho Mtakatifu.

Mama Elyapunda Mwingira, mke wa Nabii na Mtume Josephate Mwimgira
Utakatifu ni uamuzi wa mtu binafsi, ukiamua na kusema sasa naamua kuishi maisha ya utakatifu utafanikiwa katika maiasha yako na kuona Baraka za Mungu zikikuujia, ukiwa na ule utakatifu utakuwa na kila kitu unachotaka.
Tunatamani kuona utakatifu kwa waimbaji ili watakaposimama kabla hawajaimba watu wanabubujika. Mwimbaji hutakiwi kuwa na vitu vingi ambavyo havimpendezi Mungu ndani yako, kumbuka wewe ni hekalu la Mungu.

Unapokuwa Mtakatifu unazungukwa na Malaika wa Bwana. Utakatifu unaenda na Neno la Mungu. Ukiamua sasa kuwa unataka kuwa Mtakatifu, dhambi haitakupata na shetani atakukimbia.
Kama ounashauku ya kuwa Mtakatifu mbingu inaanza kukusaidia na Mungu atahamia hapo ulipo. Takasa mahali unataka pawe patakatifu. Tengeneza mazingira yako ili Mungu ahamishie maskani yake hapo.
Tengeneza kila kiungo chako utakatifu kama vile kinywa chako, mikono yako, makalio yako, tumbo lako, akili yako na kila kiungo.
Jitambue kuwa Mtakatifu, dhamiria kutoka  moyoni mwako kuwa Mtakatifu, unatakiwa kuku Mtakatifu, na maamuzi ni yako kuwa Mtakatifu. Ukiamua kuwa Mtakatifu utawafuta wengi kwa Mungu kutokana na maisha yako kubadilika na kuwa na mafanikio. Ukiona kanisa haliongezeki ujue kuna pengo la Utakatifu. Jiandae kuwa karibu na Mungu kwa kuwa Mtakatifu.
Mungu anataka urekebisha tabia yako na uwe Mtakatifu. Mungu wetu ni Mtakatifu, na wale wenye hofu ya Mungu hawapumuziki kusema, “U-Mtakatifu”. Mungu akipewa nafasi kwa Utakatifu na sio kwa maombi tutaweza kusikia shuhuda nyingi sana jinsi Mungu alivyowatendea watu wenye hofu na kutii sheria zake. Huwezi kufanya maombi wakati wewe ni mwenye hujawa Mtakatifu, ni mchafu, halafu unategemea muujiza kutoka kwa Mungu!! Lazima tujipange vizuri kutembea na Utakatifu.
Kuna watu wanakosa utakatifu na wanamdanganya Mungu kwa kusema uongo hata madhabahuni. Utakatifu ni kutii sheria na maagizo yote tunayopewa na Mungu kwa kupitia watumishi wake au kwenda sawasawa na mapenzi ya Mungu. Tunatakiwa kutii sheria za Mungu ili tuendelee kuwa Watakatifu.
Unapobeba Utakatifu unanyamazisha kila tishio. Pasipo Utakatifu, maombi yako ni bure. Kama unapinga sheria za Mungu, milango yako ya mafanikio unaifunga mwenyewe.
Ukibeba Utakatifu unaweza kumtiisha shetani na kumnyamaziasha kimia. Hakikisha akili yako inakuwa Takatifu ili wewe uwe Mtakatifu kwa kusoma Neno la Mungu. Akili yako ikitulia utatamani kusoma Neno la Mungu kila wakati. Kama utaamua kuwa Mtakatifu kutoka ndani yako basi unaweza kufanya lolote ambalo ni jema na Mungu akakusaidia.
Soma Isaya 53, Kwa kuchubuliwa kwake na maovu yetu ya kijinga yakaondoka, na alivyojeruhiwa na sisi tumepona. Kwahiyo badilisha akili yako kwa kujaza Neno la Mungu. Tamani kuwa Mtakatifu ili watu watamani kuwa kama sisi. Tumehangaika sana kwa muda mrefu bila mafanikio kwasababu hatukuwa Watakatifu.
Lazima tukubali kuondoa kila kinachompendeza shetani. Nguvu ya Mungu ikiwa ndani yetu ni rahisi kuwaleta watu kwa Yesu, kuwa na afya, kutimiza mapenzi yake. Tukiamua leo na kusema Mungu aondoe kila kitu ambacho shetani ameweka ndani yetu naye Mungu atafanya hivyo na tutapokea Neema yake.
Tuache maisha ya kuzoea Neno la Mungu na watumishi wa Mungu, kila unapowaona au unaposoma Neno la Mungu lifanye ni jipya kwako. Usikubali kukwazika, usikubali kushindwa bali muombe Mungu akusaidie. Mungu akubariki sana na utakuwa na afya njema kimwili na Kiroho kama utatii mafundisho ya Mungu. Amen

Mwandishi
Rumafrica For All Nations
+255 715 851 523

----------------------------------------------------------------

MATUKIO KATIKA PICHA KATIKA IBADA YA KWAZA

MTUMISHI SUZY MSOFE
SOMO:WANA WA MUNGU WANATAKIWA WAWEJE
Mathayo 5:8 " Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
"
SIFA ZA WANA WA MUNGU
1. Matendo yako yataonekana kwa maana kila utakalolifanya wataliona ni jema.
2. Maneno yako yatakuwa matamu na yakumpa Mungu utukufu.
3. Moyo wako ukiwa safi unakuwa na tabia njema na kuwapendeza hata wanadamu.
4. Wanamtafuta Mungu kwa bidii na wanaongozwa na Mungu na wanakuwa na muda kwa ajili ya Mungu
5. Wanakuwa na njaa na kiu ya neno la Mungu.
6. Wanatamani wengine waingie kwa Yesu ili waone uzuri wa Mungu.
7. Wana wa Mungu wakiudhiwa hawakasiriki, kwa sababu wao wanamtanzama Mungu anasema nini.


Pichani: Efatha mass choir wakimwimbia na kumtukuza Mungu wetu mkuu katika Ibada ya kwanza. Mungu wetu anatamani tumuabudu katika Roho na kweli.




Eneo maalum la maombi kwa waliofungwa na vifungo mbalimbali vya kipepo, wakiombewa na kufunguliwa, kwa Jina la Yesu.



MAMA ELIYAKUNDA MWINGIRA Akisalimia kanisa katika Ibada ya kwanza.
 




Comments