RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFTAHA MWENGE: UJASIRI NI MUHIMU KATIKA MAFANIKIO

Rumafrica ilibahatika kuhudhuria ibada ya pili inayoaanza saa 4:00 asubuhi siku ya Jumapili 22/03/2015 katika kanisa la Efatha Mwenge kwa Mtumishi wa Mungu, Nabii na Mtume Josephate Mwingira na kujifunza mengi kwa kupitia Mchungaji Thadeo Mushi. Somo lilikuwa kama ifuatavyo

Pichani: Mchungaji Thadeo Msuya akihubiri kwenye Ibada ya pili, Efatha Mwenge Dar es salaam.

UJASIRI NI MUHIMU KATIKA MAFANIKIO
Tusome Joshua 1:7, Mafanikio yameruhusiwa kwako wewe, sasa pokea nguvu ya ujasiri ili ufanikiwe. Unapokuwa na ujasiri unakuwa na uwezo wa kufikiri kufanikisha lile jambo unalofanya. Baraka zako ziko katika eneo lako la kuabudia na hapo panahitajika wewe kuwa na ujasiri wa kufanya makubwa katika eneo lako la kuabudia

Ukiwa ujasiri unakuwa smart au makini kwa kila jambo. Unapotumika katika huduma yako lazima kuwa na malengo uliyoyapanga, kwahiyo unatakiwa kuwa na ujasiri wa kupambana na vikwazo. Anza kuwa jasiri na kuondokana na woga, nenda katangaze Neno la Mungu.

Ukiwa jasiri fedha zinakufuata kwani unakuwa umedhamiria kupata kile ulichokusudia bila woga. Ondoa ile hofu ya kuogopa kukemea uovu ulio mbele yako, uwe jasiri na kuachana na woga na hofu.

Baba yetu ni mshindi kwasababu anaujasiri, sasa na wewe fanya jambo fulani ambalo litaonyesha kuwa wewe ni jasiri. Panga mipango yako na uitekeleze tena bila ya kuwa na woga.

Sisi kama wanadamu kuna vita tunapambana navyo kwahiyo inatakiwa kuwa na ujasiri wa kushinda hivi vita. Hutakiwi kuwa na woga, bali fanya kufuatana na mapenzi ya Mungu. Watu tumekuwa na maneno mengi na tumekuwa wavivu wa kufanya kazi. Tunatakiwa kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii na tunaitumikia madhabahu ya Bwana kwa ujasiri. Unatakiwa kuwa na neema ya ujasiri wa kumshughulikia adui katika mwaka huu wa mtembeo na Mungu.

UJASIRI ni nguvu iliyo ndani ya mtu kufanya jambo bila ya woga. Nguvu ya Mungu inahitajika ndani ya maisha yako ili uwe jasiri. Kama hujui siri za Mungu na kuwa mtii hutaweza kuwa jasiri. Kuna nguvu ya ujasiri ambayo tukiwa nayo tutashinda jambo lolote.

Hutakiwi kulala mpaka kile ulichokuwa unahitaji kimetimia, na hii inafanyika kwa kutii mamlaka ya Mungu. Maombi yako yasiwe kelele mbele za Mungu, ila jitahidi kuwa na ujasiri wa kufanya maombi na kutubu dhambi zako na kutorudina kuzifanya tena. (uwe mtu wa toba)

Kinyume cha UJASIRI ni uvivu. Kwahiyo yuache uvivu wa kufanya kazi. Ukiondoa uvivu hakuna jambo litakalo kushinda.

UJASIRI ni ile hali ya kung'ang'ania mpaka jambo litimie. Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu. Kubali kung'ang'ania mpaka kile ulichotaka kitokee kinatokea. Ukiwa na ujasiri ni lazima kusimamia maagizo ambayo ni sheria na kuyatekeleza.

Mwisho nasema maombi yako yawe ni maombi ya UJASIRI na ikiwezekana yawe tofauti na ya watu wengine. MUNGU AKUBARIKI SANA

-----------------------------------------
IBADA YA KWANZA


Mchungaji Mary Abel wa Eneo la Utukufu aliyeongoza Ibada ya Neno katika Ibada ya Kwanza..

Watumishi wa Mungu kwa utulivu wakifuatilia Ibada ya Neno iliyoongozwa na Mchungaji Msuya.


Efatha Mass wakimuimbia Mungu wetu, hakika wameimba kwa uzuri wa aina yake Mungu azidi kuwapaka mafuta kwa ajili ya utumishi wao. Amen

Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira naye yupo katika Ibada hii ya kwanza ni Baraka ya pekee kuwa na Baba yetu. Amen

USHUHUDA
Hery Jackson, namshukuru Mungu kwa kunipa kibali fanya kazi yake Precious Center Kibaha, baada ya kufanya kazi kwa uaminifu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alinikabidhi kwa mtu mmoja akamwambia nenda na huyu kijana ukamfundishe kazi mpaka kitu kitokee, kweli baada ya hapo niliendelea na huyo mtu niliepewa akawa ananifundisha kazi ya uhandisi wa majengo na barabara na kweli kimetokea kitu kama baba alivyosema. Sasa nafanya kazi katika makapuni mbalimbali kama Mhandisi namshukuru Mungu kwa maana kwa elimu niliyonayo nisingeweza kufanya kazi kama hii ila ni kwa neema tu. Pili namshukuru Mtume na Nabii na mchungaji wangu Aimana Dominick kwahiyo nimekuja kushuhudia haya Mungu aliyonifanyia ili kuujenga ufalme wake, Amen.



Comments