RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO YA MAZISHI YA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA THE UNIT FAMILI MAREHEMU MAGRETH MKAMA AMEAGWA SIKU YA JUMAMOSI 29.03.2015 JIJINI DAR

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wapenzi wa nyimbo za Injili siku ya leo walibaki na simanzi kubwa sana, baada ya kuhakikisha kwa macho yao ndugu yao na rafiki yao Marehemu Magreth Mkama akiwa katika nyumba yake ya milele. Machozi na vilio vilitanda kwa waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na wananchi kwa ujumla hasa pale walipoweza kushuhudia mwili wa marehemu ukiwa katika jeneza, watu wengi hawakuamini kutoka na vile marehemu alivyoweza kuishi wa watu vizuri hasa awapo katika huduma na kazi zake za kila siku.

Madamu Ruti (kulia) na Mc Sarah Mvungi wakiwa na huzuni. Hawa wako katika kundi la waimbaji ambako marehemu alikuwa naye mwanakikundi ambacho kinaitwa THE  UNIT FAMILY

Marehemu Magreth Mkama aliyezaliwa 1986 na kufariki 2015 alikuwa amejiunga na kikundi cha waimbaji kinachoenda kwa jina la THE UNIT FAMILI akiwa kama katibu wa kikundi. Marehemu ambaye alikuwa mcheshi sana kwa marafiki zake na majirani zake ameacha wanae wawili hapa duniani.

Hakika hatutamuona tena Magreth Mkama katika dunia hii mpaka siku ile ya mwisho ambayo kila mtu atatoa hesabu mbele za Mungu. Mungu akubariki sana

 Kutoka kushoto ni waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka katika kundi alilokuwepo marehemu Magreth Mkama la THE UNIT FAMILY-Kutoka kushoto ni Sarah Mvungi akifuatia Madam Ruti
 MC Joshua Makondeko akiongea

 Madam Ruti wa pili kutoka kushoto







 Madam Ruti akitokwa na machozi akiwa ameshikiliwa na Sarah Mvungi

 Jamani madamu Ruti wa Jana Imepita akilia kwa uchungu

 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Mess Jacob Chengula wa tatu kutoka kulia akiwa na huzuni



Madam Ruti

Mc. Joshua Makondeko na ni mwimbaji wa nyimbo za Injjili Tanzania

 Mtangazaji wa Praise Power Radio-Christina Mtua











Comments