RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WATU WAMIMINIKA KATIKA TAMASHA LA SIMULIZA LA VERONICA FRANK SIKU YA JUMAPILI 29.03.2015 NA KUVUNJA GETI WAKING'ANG'ANIA KUINGIA NDANI YA UKUMBI WA PRINCES HALL SINZA MAPAMBANO -DAR

Tamasha la Simulizi la Veronica Frank ambalo lillienda kwa jina la TAMASHA LA ALAMA ZA NYAKATI NA VERONICA FRANK liliwashangaza wakazi wa jiji la Dar es Salaam. Watu walikuwa ni wengi sana, yapata masaa kama matatu watu wako kwenye foleni wanasubiria kupata tiketi zao ili waweze kuingia ndani kumsikiliza Lady V (Veronica Frank). Dada huyu Mungu ameweka kitu cha pekee sana ambacho ni tofauti sana na watu wengine.

Kwako wewe ambaye hujamjua Veronica Frank, huyu ni mtangazaji wa kipindi cha ALAMA ZA NYAKATI katika redio moja ya Kikristo ya Praise Power iliyoko Mikocheni jini dar es Salaam Tanzania. Katika historia yake ni kwamba Veronica Frank kabla ya kuwa mtanagzaji alikuwa ni sekretari wa kawaida sana. Alitamani sana kuwa mtangazaji na baadae aliamua kumfuata mtangazaji wa Praise Power wa kipindi cha Alama za Nyakati enzi hizo  Bwana Erick Martini na kutaka kufundishwa kuwa mtangazaji, Erick Martin naye akamkubalia kumfundisha. Erick Martin alikuwa akitangaza kipindi hiki cha Alama za Nyakati ambacho kwa sasa Veronica Frank anatangaza kuanzia saa 12:00 alfajiri.

Kipindi hiki cha Alama za Nyakati husimulia habari za kweli kuhusiana na watu wenye mapito magumu sana na baadae Mungu kuwainua na kuwa watu wa tofauti sana kimaisha. Dada huyu anaposimulia hubeba uhusika wa jambo na watu hutamani sana kumsikiliza. Habari zake anazosimulia ni za kweli kabisa.

Siku ya jana aliweza kufanya tamasha lake kubwa sana ndani ya ukumbi wa Princes Hall Sinza Mapambano na kuwaleta watu ambao amekuwa akitoa shuhuda zao za kimaisha, jinsi gani walivyopitia mpaka sasa walipo. Kati yao alikuwepo, Erasto, Magadalena na wengine wengi sana. Ushuhuda wa Erasto ulionekana kugusa mioyo ya watu wengi sana na alipokuwa ametajwa kuja kusimulia maisha yake watu walishangalia sana na wengine kulia.

Tamasha hili lilianza saa 8:00 mchana na kumalizika saa 2:00 usiku. Cha kushangaza ni pale tu watu walioweza kusukuma lile geti na kuweza kuingia bila ya kulipia, baada ya tamasha kuisha waliweza kutoa zile pesa huku wakinga'ang'ania kumgusa Veronica Frank na Erasto ili wabate upako waliokuwa nao.

PICHA ZA VERONICA FRANK AKIWA KATIKA OFISI YA RUMAFRICA AKISUBIRIA KUCHUKUA TIKETI ZAKE SIKU YA JUMAMOSI KWAAJILI YA TAMASHA LAKE LA JUMAPILI.
Veronica Frank akiongea na Rumafrica kuhusiana na tamasha lake, alisema, "Kaka Rulea nimeota kuna watu wengi sana wakiwa na furaha sana, naomba sana Mungu kesho isinyesha mvua, naamini watu watakuwa wengi sana" Hii inaonyesha kuwa Mungu aliweza kuongea naye katika ndoto na kumpa ujasiri wa kuweza kutimiza ndoto zake na kuua kiu ya watu waliokuwa wakitamani sana kwaona watu aliokuwa akiwasimualia katika kipindi chake cha Alama za Nyakati. Pia aliweza kuonyesha wasiwasi wa tiketi zake ambazo ali-plan kuwa na tiketi 400 tu huku akiwa na wasiwasi kutozimaliza zote, alisema, "Kaka Rulea naona hizi tiketi ni nyingi sana ila zitanisaidia tamasha lingine zikibaki" Kama designer niliamua ku-design tiketi na kuacha nafasi ya kujaza maelezo mengie katika tiketi hiyo kwa siku nyinge.
Mtangaza wa Praise Power Veronica Frank wa kipindi cha Nyakati akiwa katika ofisi ya Rumafrica siku ya Jumamosi akisubiri kuchukua tiketi zake kwaajili ya tamasha lake la Jumapili
 Kushoto ni Veronica Frank aliangalia bango lake lililotengezwa na Rumafrica (+255 715 851 523) 
 Tiketi za 5,000 zikiwa zimezagaa mezani kwaajili ya Jumapili

 Veronica Frank akiwa ameshikilia tiket kabla hajakatwa kwaajili ya tamasha lake

PICHA ZA WATU WAKIWA WAMEJIPANGA FOLENI KUINGIA KATIKA TAMASHA LA LA SIMULIZI LA  ALAMA ZA NYAKATI LA NA VERONICA FRANK.

Watu walikuwa wengi sana kama utakavyowaona katika picha hapao chini, Rumafrica ilibahatika kuongea na baadhi ya watu waliofika siku hiyo kutaka kujua juu ya Veronica Frank. Baadhi yao walisema, ni kutokana na usimulizi wake, kwani akiwa anasimulia hubeba ule uhusika na pengine watu hujua ni yeye katendewa. Pia sauti yake na heshima yake. Mbali na hapo ni vile anavyoweza kuwatafuta watu wenye shida na kuweza kuwatangaza na baadhi ya watumishi wa Mungu kuweza kuwasaidia.


 Eneo la kuchukulia tiketi






PICHA WATU WAKIWA NDANI YA UKUMBI WA PRINCES HALL SINZA MAPAMBANO-DAR KATIKA TAMASHA LA KIHISTORI LA ALAMA ZA NYAKATI NA VERONICA FRANK.
Kumbe unaweza ukawa hujulikani, ila watu wanatambua mchango wako. Hii ilimtokea Veronica Frank kwa mara ya kwanza kufanya tamasha kubwa sana ambalo hakuna mtu aliweza kufanya zaidi ya matamasha ya Msama Promotion ambayo hufanyika Uwanja wa Taifa. Watu wengi hutamani sana kuwaona waiombaji wakiimba na ndio maana hufika katika matamasha yao, lakini Veronica Frank sio mwimbaji bali yeye hujifungia studio akitangaza kupitia kipindi cha Alama za Nyakati juu ya maisha ya watu na mapito yao. Watu wengi hawajawahi kumuona mtangazaji huyu kutoka na kutojionyesha kulingana na kazi yake.

Mtangazaji wa kipindi cha Alama za Nyakati Praise Power Radio- Veronica Frank
Mungu aliweza kumfanyia Sapraizi ya ajabu sana na kum-appreciate kile anachokifanya katika huduma yake ya utangazaji. Tamashi lilikuwa la kipekee sana, eneo lilikuwa na uwepo wa Mungu. Watu walionekana ni watu wakupendana ndani ya ukumbi kama ndugu, Kulikuwa na amani na utulivu wa kutosha. Hakika Mungu wa Veronica Frank atabaki kuwa Mungu tu.
 
Watu wakiwa wamebanana (aliyesimama ni mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga)

Veronica Frank
 Hii ni hatariiii

Mtangazaji wa kipindi cha Alama za Nyakati Praise Power Radio- Veronica Frank
 Baadhi ya watu walikosa eneo la kukaa na kuwalazimu kupanda ngazi na kukaa huko, nyuma ya ukumbi

Mtangazaji wa kipindi cha Alama za Nyakati Praise Power Radio- Veronica Frank
 Watu baada ta kukosa viti na eneo la kukaa wakaamua kuvamia ukuta

Mtangazaji wa kipindi cha Alama za Nyakati Praise Power Radio- Veronica Frank
 
Mtangazaji wa kipindi cha Alama za Nyakati Praise Power Radio- Veronica Frank
 MC. Joseph wa Praise Power akizidi kuhamasisha watu

Mc. Bony Magupa (Mtangazaji wa Praise Power na Channel Ten) na Veronica Frank (kulia)
 Baadhi ya watu wakinyang'anaya viti

Mc. Bony Magupa (Mtangazaji wa Praise Power na Channel Ten) na Veronica Frank (kulia)

VERONICA FRANK AKIMSHUKURU ERICK MARTIN KWA KUMFUNDISHA UTANGAZAJI NA KUMRITHISHA KIPINDI CHA ALAMA ZA NYAKATI PRAISE POWER
 Erick Martin (kushoto) na Veronica Frank
 Meneja wa Praise Power Radio George Mpella (kushoto)
  Meneja wa Praise Power Radio George Mpella

Ma-MC. Bony Magupa (BM) kulia na Joseph-wote ni watangazaji wa Praise Power Radio

KIPINDI CHA WAIMBAJI KUMTUKUZA MUNGU KWA NJIA YA UIMBAJI
 Magadelea
 Chistopher Mwahangila


Beatrice Mwaipaja


Edson Mwasabwite wa Ni Kwa neema na Connection

Edson Mwasabwite wa Ni Kwa neema na Connection

Mwimbaji Tumaini Njole (kulia) na Veronica Frank


Unknown

KIPINDI CHA KUWATAMBULISHA WATU ALIOKUWA AKIWASIMULIA KATIKA KIPINDI CHAKE CHA ALAMA ZA NYAKATI-PRAISE POWER RADIO






PICHA ZIMEPIGWA NA RUMAFRICA +255 715 851 523
MATUKIO MENGINE BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KULIA.




















































































Comments